Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein , Aaza Ziara yake Katika Mkoa wa Mjini Magharibui Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud wakati alipowasili katika viwanja vya zamani vya Baraza la Wawakilishi Kikwajuni kupokea Taarifa za Utekelezaji wa Kazi za Serikali katika Mkoa wa Mjini Magharibi kabla ya kuaza ziara yake katika mkoa huu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiangalia ngoma ya MwanaNdege akikaridishwa katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuaza ziara yake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Waziri Kiongozi Mstaaf Mhe. Shamsi Vuai Nahodha alipowasili katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi la zamani kuaza ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akimkabiti Taarifa ya Utendaji Kazi ya Mkoa wa Mjini Magharibi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, kabla ya kuaza ziara yake iliosomwa katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akihutubia na kutowa nasaha zake kwa watendaji wa SMZ wa Mkoa wa Mjini Magharibi kabla ya kuaza kwa ziara yake katika mkoa huo.
Waheshimiwa Wabnge na Viongozi wa Serikali na Watendaji wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwahutubia kabla ya kuaza ziara yake katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.