Habari za Punde

Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi wa Serikali alipowasili katika Majengo ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kusini Tunguu Unguja kupata maelezo ya Utelelezaji wa Maendeleo ya Mkoa huo kabla ya kuaza ziara yake kutembelea Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhali Ali Kichupa alipowasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk Ali Mojhamed Shein, akitia saini kitabu cha wageni alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Afisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja kupata taarifa za Utendaji wa Kazi katika Mkoa huo.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe Kitwana Idrisa Mustafa akisona taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiazia ziara yake hapo baada ya kupata taarifa hiyo. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Haji Omar Kheri akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuzungumza na Watendaji wa Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa ziara ya Rais katika Mkoa huo. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Kusini baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa huo uliosoma kabla ya kuaza ziara yake. 
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.