Habari za Punde

Jamii yakumbushwa kupima afya mara kwa mara na kujiunga na vikundi vya mazoezi

Na Mwashungi Tahir         Maelezo 

JAMII imetakiwa ijenge mazowea  ya kufika katika vituo vya afya mara kwa mara  kwa kupima  afya zao  pia   kujiunga na vikundi vya kufanyia mazoezi  ili kujiepusha na maradhi yasiyoweza kuambukiza.

Akizungumza na vikundi vya mazoezi pamoja na wananchi wa jimbo la Mpendae Mwakilishi wa jimbo hilo Saidi  Mohammed Dimwa wakati alipokuwa akiwa katika maadhimisho ya siku maradhi ya moyo duniani.

Alisema  hivi sasa takribani duniani kuna wimbi kubwa ya maradhi yasiyoambukiza ikiwemo shindikizo la damu, sukari na moyo  hivyo aliwaomba wananchi wajenge tabia ya kufanya mazoezi ili waweze kuepukana na maradhi hayo.

Amewataka jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza ZNCD  kuzidi kutoa elimu  na kuwashajihisha wananchi kuacha kula  sana  vyakula vya mafuta  na kupendelea zaidi kula matunda na mboga mboga kwa lengo la kulinda afya zao.

Pia amewaomba watu waache tabia ya uvutaji wa sigara , tumbaku  pombe na madawa ya kulevya   kwani vitu hivi ndio sababu kuu ya kupatikana maradhi hayo.

“Wizara ya Afya tayari imeweka  kanuni ya uvutaji wa sigara na tumbaku ambapo hivi sasa  inaanza kuifanyia kazi  kwa kuchukuliwa hatua wale wanaovuta hadharani”Alisema Dimwa.

Vile vile amewataka wananchi  iwapo baada ya kuchunguza afya na kubainika kuwa wamepata maradhi hayo kufika vituo vya afya kwa kupatiwa ushauri na kutumia dawa kwa uangalifu.

Nae msoma risala wa jumuiya hiyo Mkubwa Ibrahim Khamis amesema hivi ssa ongezeko la maradhi yasiyoambukiza Zanzibar yamefikia asilimia 33 hivyo amewahimiza wananchi wawe na uzoefu wa kufanya mazoezi ili kupunguza mwili na kujenga afya zao. .

Sambamba na hayo mwakilishi wa jumuiya ya watoto wenye ugonjwa wa moyo Abdulwahab Moh’d Suleiman  amesema zaidi ya watoto 750 wenye maradhi hayo wanatibiwa nje ya nchi .

Alisema uwepo kwa jumuiya hii Zanzibar ni kufikia malengo kwa kutoa mahitaji maalum  kwa watoto hao na kufahamu uwepo wa chombo mbadala  na kupatiwa mahitaji  yao ya lazima  katika matibabu.

Ujumbe wa mwaka huu Linda moyo wako kwa kula vyakula bora na kufanya mazoezi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.