Habari za Punde

Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Azungumza na Waandhi wa Habari Kukamilika kwa Maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Baraza la Tisa Wawakilishi Linaloanza Kesho Zanzibar. 27/9/2017

 Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Raya Issa Mselem akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbambali vilioko Zanzibar kutoa taarifa ya kukamilika kwa Mkutano wa Saba wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar unaotarajiwa kufanyuika kesho katika ukumbi wa baraza Chukwani Zanzibar. 
Katika Mkutano huo kutawasilishwa maswala na kujibiwa 136 yataulizwa na Wajumbe wa Baraza na kusomwa kwa mara ya Pili Miswada ya Sheria, iliosomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Baraza wa mwezi wa Mei -June 2017.Na kusomwa kwa mara ya Pili kesho na kujadiliwa na Wajumbe wa Baraza katika mkutano huo unaoaza kesho.
Miswada itakayowasilishwa ni Mwaswa wa Sheria kufuta Sheria ya Mahkama ya Kadhi Nam.3 ya mwaka 1985 na kuanzisha Upya Mahkama ya Kadhi na kuweka masharti mengine yanayohusiana na hayo 
Mswada wa Sheria wa kuazisha Baraza la Taifa la Biashara na Kuweka mambo mengine yanayohusiana na hayo .Pia itawsilishwa Ripoti ya Wizara za SMZ kuhusiana na utekelezaji wa maagizi ya Kamati za Kudumu za Baraza.
Kuwasilishwa Ripoti ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) 
Katibu wa Baraza Raya Issa Mselem amesema itawasilishwa kwa mara kwanza Miswada mbalimbali katika mkutano huo itasomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Saba Baraza la Tisa.
Mshauri wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mussa Kombo Bakari akitowa ufafanizi maelezo na kujibu maswali yalioulizwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na Mkutano wa Saba Baraza la Tisa unaoaza kesho Zanzibar kwa wajumbe kuuliza maswali 136 na kujibiwa na Mawaziri husika na kusomwa kwa mara ya Pili Miswada ya Sheria.
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo na Katibu wa Baraza la Wawakilishi Raya Issa Mselem akitowa taarifa ya kukamilika kwa maandalizi ya mkutano huo unaoanza keshio katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.