Habari za Punde

Kocha King Ajiuzulu Kuifundisha Kombaini ya Mjini.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha mkuu wa timu ya Soka ya Kombain ya Mjini Unguja  Mohammed Seif “King” amejiuzulu kuifundisha timu hiyo baada ya kupata mafanikio makubwa kwa miaka 3 mfululizo tangu alipoanza kuifundisha kikosi hicho .

Sababu kubwa iliyomfanya akae pembeni kocha huyo ni mafanikio makubwa aliyoyapata na kusema kwasasa anawapa nafasi makocha wengine kuifundisha timu hiyo.

“Nawapa nafasi makocha wenzangu kuifundisha timu hii, nimeongoza kwa mafanikio makubwa, kwasasa nimeamua kukaa pembeni kwani hapa Wilaya ya Mjini kuna makocha wengi bora na wenye sifa ya kuifundisha timu hii, sasa ni fursa na wao kwao kwani mimi nimeongoza kwa mafanikio makubwa”. Alisema King.

Kocha King alianza kuifundisha timu hiyo tangu mwaka 2015 ambapo alitwaa kombe la Wilaya za Zanzibar, mwaka 2016 akatwaa Ubingwa kwa mara ya kwanza kwenye Mashindano ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati ya Rolling Stone ambapo Mjini Unguja walishinda kombe hilo kule Arusha na mwaka huu 2017 akashinda tena kombe hilo huko wilayani Mbulu Mkoani Manyara.

Kwasasa Kocha huyo anafundisha timu ya Miembeni City ambayo inashiriki ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.