Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Atembelea Maonyesho Kabla ya Kuzindua Mpango wa Muongozo wa Matumizi ya Maji Usafi wa Mazingira Kwa Wanafunzi wa Skuli za Msingi Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Kiembesamaki Zanzibar kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa Mpamgo wa Muongozo wa Matumizi ya Maji Usafi na Mazingira kwa Wanafunzo wea Skuli za Msingi Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF Tanzania Rene Van Dongen, alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Kiembesamaki kwa ajili ya uzinduzi huo wa mpango uliofadhiliwa na UNICEF kwa ajili ya Wanafunzi wa Skuli za Msingi Zanzibar. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Vitambu mbalimbali wakati wa hafla hiyo akipata maelezo kuoka kwa Mwanakilishi wa banda hilo la Save The Children Zanzibar Maruzuku Mussa. 
Mwakilishi wa banda la maonesho la ZANREC Asia Mwadini Mohammed, akitowa maelezo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipotembelea banda hilo kujionea uhifadhi na ubadilishaji wa takataka kuwa mali hafi na vifaa vya kutumia, akishika moja ya bidhaa hiyo itokanayo na chupa na kutegenezwa glass na vifaa vya mapambo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia moja ya bidhaa zitokanazo na bidhaa zinazotokana na majumbani na mahotelini chupa ikiwa imegeuzwa kuwa matumizi ya taa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea banda la ZOP wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya skuli ya msingi kiembesamaki.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.