Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuwait kwa Maendeleo ya Kiuchumi ofisini kwake Vuga
Picha ya pamoja iliyopigwa baada ya ujumbe wa Mfuko wa Kuwait kwa Maendeleo ya Kiuchumi kupokea neno la Shukrani kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar (kulia ni Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Khalid S. Mohammed na kushoto ni Naibu wa Mfuko wa Kuwait kwa Maendeleo ya Kiuchumi Bwana Hamad s. Al Omar )
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya Mlango (Zanzibar door) Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Kuwait kwa Maendeleo ya Kiuchumi Bwana Hamad S. Al Omar baada ya kuwezesha kusainiwa kwa mkataba wa Mkopo kwa ajili ya ukarabati mkubwa wa hospitali ya Mnazi Mmoja.
Na Sharifa Barki Juma, OMPR
Mheshimiwa
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd akutana na Uongozi wa Mfuko wa
Kuwait Kwa Maendeleo ya Kiuchumi ofisini kwake Vuga kwa lengo la kutoa neno la
Shukrani baada ya kupatiwa mkopo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
ajili ya Mradi wa Ukarabati Mkubwa wa Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Balozi
Seif alitoa shukrani hizo za dhati kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar baada ya Serikali kupatiwa fursa ya kusaini Mkataba wa Mkopo huo chini
ya Uongozi wa Mfuko wa Kuwait unaongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo Bwana
Hamad S. Al Omar.
Kiasi
cha Fedha kilichosainiwa na Mheshimiwa Waziri
wa Fedha na Mipango Dr. Khalid S.
Mohamed ni dola za kimarekani Milioni
elfu kumi na tatu nukta sita ambazo ni sawa na
zaidi ya Bilioni thelathini za kitanzania kwa ajili ya kuchangia
sehemu ya ukarabati mkubwa wa hospitali hiyo.
Sambamba
na hayo Mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais amemuomba Naibu Mkurugenzi wa Mfuko
wa Kuwait kuzidi kuipa fursa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutoa mikopo
kwa lengo la kuendelea kuchangia sekta
mbalimbali za kimaendeleo nchini zikiwemo uchumi, elimu na jamii kiujumla.
Balozi
Seif ameuambia ujumbe huo kwamba Zanzibar ni nchi yenye amani, upendo na
utulivu hivyo hufungua milango ya fursa kwa wawekezaji kuja kuwekeza nchini
hapa.
Pia
wageni wengi huvutiwa na utulivu wa nchi hii jambo ambalo linapelekea kuwepo
kwa wageni kutoka nchi mbali mbali duniani kwa lengo la kuekeza na kuiendeleza
nchi yetu.
Mheshimiwa
Makamu wa Pili wa Rais aliusisitiza ujumbe huo kuwa mlango wa Zanzibar uko wazi kwa mtu
yeyote ambae yuko tayari kuja kushirikiana nasi kwa lengo la kusukuma gurudumu
la maendeleo ya nchi yetu.
Nae
Naibu Mkurugenzi wa mfuko wa Fedha wa Kuwait amesema nchi yake iko tayari
kujitolea kwa maendeleo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo
kusaidia sekta ya elimu, afya na nyenginezo.
Nchi
hiyo pia iko tayari mda wowote kuanzia sasa kutoa msaada kwa kila jambo kwa
lengo la kukuza mashirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili na uboreshaji wa
maeneo ya ushirikiano huo baina ya Zanzibar na Mfuko wa Kuwait.
No comments:
Post a Comment