Habari za Punde

Mrajis wa michezo Zanzibar awataka ZAHA waachane na majunguNa: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Chama cha Mpira wa Mikono Zanzibar yani Hand ball (ZAHA) wametakiwa kuachana na majungu na badala yake kuwa na umoja na mshikamano ili kuukuza mchezo huo.

Kauli hiyo imetolewa na Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar, Suleiman Pandu Kweleza, ambapo pia amewasisitiza kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali kwenye uachaguzi wa chama hicho ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kweleza amesema umoja wao ndio silaha ya kuukuza mchezo huo ambao unanafasi kubwa ya kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwenye anga za Kimataifa.

“Hand ball mimi nawaomba waendelee kuwa na umoja waache majungu mana kuna baadhi yao huwa wanalalamika, sasa washirikiane na katika uchaguzi washiriki kugombea na si kusubiri viongozi wapya kasha kuwapiga majungu ambayo hayana faida yoyote”. Alisema Kweleza.

Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) kupitia Afisi ya Mrajis wa vyama vya Michezo Zanzibar bado linaendelea na mchakato wake kwa vyama vyake vilivyokuwa havijanya Uchaguzi vifanye haraka ambapo kwa mwaka huu tayari zaidi ya vyama 4 tayari vimeshafanya Uchaguzi.

Vyama hivyo vilivyofanya Uchaguzi mwaka huu ni Chama cha Mpira wa Ukuta Zanzibar “Zanzibar Squash Racket Association (ZSRA)”, Chama cha Mpira wa Kikapu Zanzibar yani Basketball (BAZA), Chama cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA) na Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar yani Table Tennis (ZTTA) ambapo kwasasa BTMZ wapo mbioni kuhakikisha chama cha Chama cha Hand Ball Zanzibar kinafanya uchaguzi pamoja na Chama cha Karata, Bao, Chama cha Baskeli Zanzibar (CHABAZA) na Chama cha Riadha Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.