Habari za Punde

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Harusi Atembelea Bohari la Kuu la Madawa na Kukuta Dawa za Kutosha.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo, iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi. Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo, iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga.
Na Mwashumgi Tahir. Maelezo, Zanzibar .
SERIKALI ya  Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa Bohari kuu ya Dawa inadawa za kutosha za kuhudumia wagonjwa wanaofika kupata matibabu katika Mahospitali na vituo vya Afya.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakati alipofanya ziara katika Bohari kuu ya Dawa na kuangalia namna ya upatikanaj i wa dawa.

Amesema uwepo wa Dawa katika Bohari kuu ya dawa nikuonesha kuwa Serikali   ina imani na wananchi wake kwa kuongeza Bajeti ya ununuzi wa dawa kwa asilimia mia moja ambapo upungufu upo kidogo kwenye dawa za wagonjwa wa akili ambap o Wizara iko mbioni kutatua tatizo hilo.

”‘Wananchi msininuwe dawa katika mahospitali na vituo vya Afya zipo za kutosha  kwani Serikali imefanya jitihada kubwa ya kueneza dawa na kuzisambaza mahosptalini    mote na vituo vya afya ambapo kama kutakuwa na upungufu wa  dawa  Wizara tutatoa taarifa maalum kwa wananchi wake”. Naibu Waziri huyo Alisisitiza.

Amewataka wafanyakazi wa Mahospitalini na Vituo vya Afya kuagiza dawa kwa wakati kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondosha urasimu kwa wagonjwa ambao wanaokwenda kupata huduma ya matibabu na kuwambiwa dawa hakuna ambapo kuna dawa za kutosha katika Bohari ya dawa.

Kwa upande wa Mkurugenzi Bohari kuu ya Dawa Zahran  Ali  Hamad amesema kwa mujibu wa mahitaji ya dawa muhimu zinazotumika katika visiwa vya Unguja na Pemba dawa zipo za kutosha kwa kuwahudumia wananchi.

Amezitaja dawa hizo ni pamoja na za akinamama wanofika kujifungua,dawa za mpango wa uzazi, dawa ya kisukari na pressure na maradhi mengine na kuwasisitiza wahudumu wa afya kuagiza dawa  kwa wakati.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.