Habari za Punde

Rais Alhajj Dkt. Ali Mohamed Shein, Afungua Mskiti Mpya wa Kisasa wa Masjid Jaaamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar Uliojengwa na Mfalme Qaboos

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Viongozi wa Dini Zanzibar na Wawakilishi wa Mfalme Qaboos wakiwa katika viwanja vya Masjid Jaamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar wakisubiri kumpokea Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzin Alhajj Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa ajili ya Ufunguzi wa msiokiti huo ulioko katika maeneo ya mazizini jirani na Chuo cha Kiislam Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud alipowasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kuufungua msikiti huo leo ijumaa 22/9/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dkt. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Oman Nchini Tanzania alipowasili katika viwanja vya Masjid Jaamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.