STATE
HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF
THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 26.09.2017

RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za
pongezi Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping kwa kutimiza miaka 68 tokea
kuasisiwa kwa Taifa hilo.
Katika salamu hizo, Dk. Shein alimpongeza Rais Xi
Jinping kwa kutimiza miaka 68 ya Taifa hilo tokea kutangazwa rasmin na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Kikomunisti cha Jamhuri ya Watu wa China Hayati
Mao Zedong mnamo Oktoba 1, mwaka 1949.
Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar
wataendeleza umoja na mshikamano walionao kati yao na ndugu zao wa Jamhuri ya
Watu wa China kwa lengo la kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria
uliopo kati ya pande mbili hizo.
Aidha, katika salamu hizo, Dk. Shein alimtakia
sherehe njema kiongozi huyo wa Jamhuri ya Watu wa China pamoja na wananchi wake
wote sambamba na kuendeleza amani na utulivu iliyopo nchini humo pamoja na kuimarisha
zaidi mafanikio yaliopatikana katika sekta za uchumi na maendeleo.
Dk. Shein katika salamu hizo, alieleza kuwa katika
miaka 68 tangu kuasisiwa kwa Taifa hilo, Jamhuri ya Watu wa China imeweza
kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kudumu kati yake na Zanzibar.
Sambamba na hayo, Dk. Shein alimtakia kiongozi
huyo pamoja na familia yake na wananchi wote wa Jamhuri ya Watu wa China afya
njema, na mafanikio zaidi katika kuuimarisha uchumi wao ambao umekuwa
ukiimarika siku hadi siku sambamba na maendeleo yaliopo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment