Habari za Punde

Taarifa ya CCM Kwa Vyombo vya Habari.

Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kinatarajiwa kufanyika kesho Septemba 18 mwaka huu, chini ya Makamu  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Itikadi na Uenezi Mhe. Waride Bakari Jabu,  imesema kikao hicho cha siku moja kitafanyika katika Ukumbi wa Afisi kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kitapokea na kujadili kwa kina taarifa ya Hali ya Kisiasa ya Zanzibar pamoja na taarifa nyengine mbali mbali kutoka Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, vile vile kikao hicho kitapokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa CCM katika ngazi za Wilaya kwa kipindi cha 2017-2022, kwa upande wa Zanzibar na kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC - Zanzibar kilichofanyika Septemba 16, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, kwa ajili ya kuandaa Ajenda za kikao hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.