Habari za Punde

TCCIA Yazindua Malipo Kwa Njia ya Mtandao.

Rais wa TCIA akifafanua jambo mbele wa wafabiashara walioshirika katika mkutano mkuu wa mwaka.
Chama cha wafanyakazi, kilimo na viwanda Tanzania kimefanya mkutano wake mkuu wa mwaka pamoja na kuzindua   mfumo mpya wa ulipiaji bidhaa  kwa njia ya mtandao ‘LIPA FASTA’ lengo  kubwa  likiwa ni kusaidia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi. 
Mfanyabiashara na mwanachama wa TCCIA ndugu mustafa hassanal akisalimiana na mgeni rasmi  ndugu Raymond Mbilinyi katika mkutano mkuu wa mwaka, pembeni ni makamu Rais wa TCCIA ndugu Octavian Mshiu
Huduma hii imezinduliwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa TCCIA ambapo wanachama wote wa TCCIA pamoja na wafanyabiashara mbalimbali walihudhuria mkutano huo kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa huduma hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wafanyabiashara wengi. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Gotfrid Muganda akiongea na wafanyabishara waliohudhuria katika mkutano mkuu wa mwaka
Akizungumza kwenye mkutano huo  Mkurungezi  Mtendaji ndugu Gotrid Muganda alisema ‘LIPA FASTA ni mkombozi kwa wafanyabiashara wote katika kurahisisha njia zao za kufanya malipo. Kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao nje ya nchi, sasa hawana  haja ya kuwa na wasiwasi  katika kufanya malipo kwani mfanyabiashara anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake.Mfumo huu utasaidia wafanyabiashara kupata cheti cha uwasili kwa muda mfupi.
Rais wa TCCIA ndugu John Mayanja akifafanua jambo katika mkutano hu
Nae makamu wa Rais wa  chama Ndugu Octavian Mshiu amesema’ mpango huo utaendeshwa na TCCIA kuanzia ngazi ya wilaya ili kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara  wanaosafirisha bidhaa zao nje ya nchi’
LIPA FASTA ni zaidi ya njia ya malipo kwani hapa hata watanzania waishio nchi za nje ya nchi watapata nafasi ya kupata taarifa sahihi za soko, kuhifadhi taarifa sahihi za soko na bidhaa zilizopelekwa kwenye maitaifa mbalimbali pamoja na  kumwezesha mfanyabiashara kufanya malipo popote alipo.
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wakifwatila mkutano

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.