Habari za Punde

Uzinduzi wa Mbio Fupi za Marathon Zanzibar Kufanyika Tarehe 18/11/2017 Zanzibar Diabetes Marathon 2017.

Mrajisi wa Vyama vya Michezo Zanzibar Suleiman Pandu kushoto akizundua Zanzibar Diabetes Half Marathon inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao tarehe 18/11/2017 itakayoazia katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani Zanzibar na kumalizikia katika viwanja wa Amaan Zanzibar. na kuwashirikisha Wanariadha mashuhuri Duniani katika marathon hiyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Wagonjwa wa Sukari Zanzibar Ndg.Ali Zuberi akivuta kipazia kuashiria kuzindua Marathon fupi itakayowashirikisha Wagonjwa wa Kisukari Zanzibar ikiwa na Ujumbe wa Mbiu Kuu "Sukari na Mwanamke"
Viongozi wa JOMO na kutoka Wizara ya Afya Zanzibar katika Kitengo cha Magonjwa wa Kisukari wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa Marathon Zanzibar Diabetes Marathon 2017.
Meneja Masoko wa Kampuni ya JOMO International Nobert Kabendela akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Uwanja Amaan Zanzibar.na kuzungumzia Marathon hiyo itawashirikisha Wananchi wa Rika tafauti na kujumuika na Wanariadha mashuhuri wa Kimataifa watashiriki marathon hiyo.
Meneja Kitengo cha Maradhi Yasioambukiza Zanzibar Omar Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Hafl Marathon Zanzibar Diabetes Maradhon yatakayoazia katika viwanja vya Mnara wa Mapinduzi Michezani Zanzibar. ikiwa ni kuadhimisha Siku ya Wagonjwa wa Kisukari Duniani.
Mwenyekiti wa Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Zanzibar Ali Zuberi akizungumza wakati wa uzinduzi huo wa Zanzibar Diabetes Marathon inayotarajiwa kufanyika Zanzibar na kuazia katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Michezani.
Rais wa Chama cha Wanariadha Zanzibar (ZAAA) Abdulhakim Cosmas akizungumza maandalizi ya Marathon hiyo ya Kimataifa inayotarajiwa kufanyika mwezi wa Novemba 18,2017, itaazia katika viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu Michezani na kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Mrajisi wa Vyama Vya Michezo Zanzibar Suleiman Pandu akizundua Hafl Marathon kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa Uwanja wa Amaan Zanzibar na Marathon hiyo inabeba Ujumbe wa Kauli Mbio "Sukari na Mwanamke' Zanzibar Diabetes Zanzibar Marathon,


Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kisukari Zanzibar Dk Faiza Kassim Suleiman akizungumzia ugonjwa wa kisukari wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika katika ukumbi wa VIP Uwanja wa Amaan Zanzibar na kuwataka wananchi kujitokea kwa wingi Siku hiyi inayoendana na maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani kupima afya zao.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Zanzibar Mlingi Maganga Bwire akitowa neno la shukrani kwa kampuni ya JOMO kwa kufadhili Matrathon hiyoNo comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.