Habari za Punde

Watumishi na Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni watakiwa kuitumia vizuri fursa ya mafunzo

Na Khadija Khamis – Maelezo  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe,  Issa Haji  Gavu  amewataka Watumishi  Wahudumu wa Viongozi wa Serikali na Wageni   kuitumia vizuri fursa  ya mafunzo walioipata ili kuzidisha ufanisi katika kazi zao  .

Alisema ikiwa wataitumia vyema  vizuri fursa hii katika kujipatia  mafunzo ya upishi na ukarimu  wataongeza  utaalamu na kuweza kupata mbinu zaidi  ya kubadilishana uzoefu kwa namna moja au  nyengine .

Hayo aliyasema katika ufunguzi wa mafunzo ya wiki moja  ya watumishi wahudumu  wa Viongozi wa Serikali uliofanyika katika  Ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Kikwajuni  yatayoendeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China (China National research Institute of food and Fermation Industries).

Aidha alisema  mafunzo hayo yatarahisisha kutafsiri nadharia halisi zitazofundishwa na kuona uhalisia wa mambo yanavyokuwa pamoja na kubadilishana uzoefu  na kuzidisha ushirikiano .

Aliwataka washiriki kuwa makini katika  kuzingatia  muda wote wa masomo pamoja na kutoa mashirikiano  kwa wakufunzi ili waweze kuwa na ari ya ufundishaji pia wasisite kuuliza maswali iwapo watakuwa hawajafahamu, ili lengo la mafunzo hayo yafanikiwe.

“Wengi wenu bado mna umuhimu wa kutafuta elimu hasa  mkizingatia kwamba elimu haina mwisho na  ndio dira ya mafanikio katika kulipeleka mbele Taifa hasa katika wakati huu wa sayansi na teknolojia.” alisema Waziri.

Alifahamisha jinsi ya makubaliano ambayo yaliofikiwa na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kwa kuwapatia mafunzo watendaji wake ya upishi na ukarimu  iwe chachu ya kujipatia maendeleo kwa jamii .

“Faraja urafiki na uhusiano uliodumu kwa muda mrefu uendelee kudumu  baina ya Ndugu   zetu hao  wa Serikali hizo,  “alisema Waziri Gavu .

Hata hivyo alitoa rai kwa wakufunzi hao kuweza kujifunza mambo mbali mbali ya kihistoria hapa Zanzibar na kutembelea sehemu za kivutio pamoja na kuona miti ambayo ni maarufu kwa viungo ambavyo vinatumika Zanzibar .

Nae Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China Xie Xiaowi alisema wataendelea kudumisha mashirikiano baina yao pamoja   na udugu  wao ili kuleta maendeleo ya kiuchumi na kiutamaduni katika nchi hizo .

Nae mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mvita  Khamis  alisema amefurahishwa kupata fursa hiyo ya mafunzo ya mapishi na ukarimu anatarajia akimaliza  atayatumia ipasavyo kwa uweledi mkubwa  katika kutoa  huduma bora kwa Viongozi na wageni .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.