Habari za Punde

JKU yabeba ngao ya Hisani

 Kikosi cha Timu ya JKU kilichotwaa ngao ya Hisani
 Kikosi cha Miembeni City
Ngao ya hisani


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

TIMU ya JKU imefanikiwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kuashiria ufunguzi wa msimu mpya wa 2017-2018 wa Ligi Kuu ya Soka visiwani Zanzibar baada ya ushindi wa wa mabao 2-0 dhidi ya Miembeni city katika Uwanja wa Amaan jioni ya leo.

Mabao ya JKU yamefungwa na Salum Mussa dakika ya 47 na Nassor Mattar dakika ya 48.

Baada ya mchezo huo, maana yake pazia la Ligi Kuu ya Soka visiwani Zanzibar ndiyo limefunguliwa rasmi na ligi hiyo itaanza rasmi Oktoba 3, 2017 ambapo mechi za awali zitakua kama ifuatavyo.
3/10/2017
Mafunzo Vs JKU saa 8:00 mchana

J/Boys Vs KMKM saa 10:00 jioni4/10/2017

Kilimani City Vs Kipanga saa 8:00 mchana

Charawe Vs KVZ saa 10:00 jioni5/10/2017

Zimamoto Vs Taifa J saa 8:00 mchana

Polisi Vs Miembeni C saa 10:00 jioni6/10/2017

Chuoni Vs Black S saa 10:00 jioni
Baada ya mzunguko huo ligi itasimama hadi tarehe 15/10/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.