Habari za Punde

Mkurugenzi Mpya Ajipanga Kuifikisha Mbali Zaidi ZANTEL

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Sherif El Barbary akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kumtambulisha Mkurugenzi huyo mpya kwa vyombo vya habari uliofanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuwahakikishia wateja wa Zantel kutarajia huduma bora zaidi na kuhaidi kuifikisha Kampuni hiyo mbali zaidi. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Joanitha Rwegasira Mrengo.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali watu Zantel, Joanitha Rwegasira Mrengo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hafla ya kumtambulisha Mkurugenzi Mkuu wa Zantel kwa waandishi wa habari iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu mpya wa Zantel Sherif El Barbary.
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Zantel, Sherif El Barbary akisalimiana na Mwandishi wa gazeti la DailyNews, Abduel Elinaza wakati wa hafla ya mkutano na waandishi wa habari iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. 


Wateja wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu Zantel wataweza kuendana na mabadiliko ya kidunia katika  sekta ya Mawasiliano kupitia mfumo ulioboreshwa wa data na sauti baada ya kumalizika kwa kazi ya uboreshaji wa mfumo mpya wa mtandao wa kisasa ili kuongeza ubora wa bidhaa na huduma kuelekea mwaka 2018.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, 
Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Sherif El Barbary alisema  amedhamiria katika kuboresha ubora wa mtandao huo na kuwafikia wateja nchi nzima na kuenea sehemu kubwa zaidi Tanzania, kwa kutoa huduma bora na kuifanya Zantel kukua katika soko la ushindani kwenye sekta ya Mawasiliano.

“Tunatarajia kuwafuata wateja wetu walipo na kuwapa kile wanachostahili ili kuhakikisha kwamba wanamudu gharama na kuongeza kipato kupitia malengo na dira yetu,” alisema.

El Barbary aliongeza kuwa, Zantel ipo katika hatua za mwisho kumalizia uboreshaji wa mfumo wa mtandao na haina shaka kwamba, imekuwa kampuni ambayo inatoa huduma bora za mtandao wa data nchini katika mikoa zaidi ya 22 ambapo wanapata mfumo ulio na kasi ya 4G, huku malengo yake yakiifanya kuongoza katika soko na mfumo mpya wa kisasa na kidigitali.

Alisisitiza kwamba Zantel itataendelea kushirikiana na Serikali ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa kila nyanja.

“Tumetengeneza zaidi ya ajira 5,000 nchi nzima. Hizi ni zile rasmi na zisizo rasmi kupitia mfumo wa EzyPesa ambapo una takribani mawakala 2,500. Pia tumekuwa tukitoa huduma mbalimbali kwa wafanyakazi wetu wa Zantel.  Hii ni tofauti na wasambazaji wetu ambao wamekuwa wakifanya kazi na watu mbalimbali kusambaza bidhaa na huduma zetu, “aliongeza.

Kwa upande wa huduma za kijamii, Zantel imekuwa ikishiriki kupitia M-Health ambayo ni taasisi isiyo ya kiserikali ambayo imekuwa ikisaidia kuimarisha sekta ya afya kwa kuboresha huduma bora za afya hususani za mama wajamzito na watoto. Kwa kuunganisha mifumo ya intaneti ya data imekuwa njia rahisi ya kutoa elimu kupitia kampeni mbalimbali.

Zantel imekuwa ikiangazia eneo jingine ambalo ni pamoja na na kufanya biashara kwa jumla na makampuni, jambo ambalo limekuwa nyenzo muhimu kwenye biashara. Zantel inasimamia njia mbili ambazo ni EASSy & SEAS ambayo ni mifumo ya chini ya bahari ambayo imepita hadi Dar es Salaam. Mifumo hii imesaidia kuliunganisha taifa kwenye mfumo wa intaneti kwa njia ya saterite inayosaidia  kusafirisha sauti na huduma za data.

Kwa kuboresha ubora wa bidhaa na huduama pamoja na na bidhaa za Ezypesa ambayo ndiyo huduma ya kwanza kuzinduliwa ambayo iliambata na huduma ya simu ya kibenki inayofahamika Mobile Islamic Banking ambayo inashirikiana na People’s Bank of Zanzibar ambapo asilimia 85 ya wakazi wa Zanzibar wanaitegemea.

“Hivyo tunaahidi mambo makubwa mazuri yanakuja kwa wateja wetu siku zijazo,” aliongeza El Barvary.

BWANA SHERIF BARBARY ALITEULIWA KUWA OFISA MKUU MTENDAJI JULAI 1, 2017
El Barbary ana uzoefu wa takriban miaka 20 kwenye sekta ya Mawasiliano, na ameshika nafasi mbalimbali za juu za utawala ambazo ni taasisi za kimataifa.
Kabla ya kujiunga na Zantel, El Barbary alikuwa Ofisa Ufundi na Mawasiliano Tigo nchini Chad tangu mwezi Machi 2016, amefanya kazi kama msimamizi wa masuala ya mtandao na shughuli za IT na ufuatiliaji. Pia amekuwa kaimu Meneja Mkuu nchini Chad kwa miezi mitatu kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu.

El Barbary amefanya kazi miaka 6 Huawei kabla ya kujiunga na Millcom akiwa kama meneja wa huduma ukanda wa Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika. Pia amekuwa kwa miaka 6 kama COO kampuni ya Glextel akihusika na usimamizi wa utoaji huduma za wireless na mtandao, ambapo alikuwa akisimamia takribani makampuni 10 yanayofanya shughuli zake Afrika na Mashariki ya Kati.

Pia amefanya kazi na Lucent Technologies na amekuwapo kwa miaka kadhaa Amerika Kusini akifanya kazi na Kampuni ya Hewlett Packard and CML Telus ambako alipata uzoefu zaidi katika masula aya biashara akiwa kama Mkuu wa Kitengo cha Channel Operations.

Sherif El Barbary anajaza nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Benoit Janin ambaye ameitumikia kampuni hii kwa mwaka moja na miezi 10. Zantel imekuwa ikifanya shughuli zake tangu mwaka 1999 ikiwa na hisa za asilimia 85  pamoja na  asilimia 15 hisa za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa Mawasiliano zaidi:
Rukia Mtingwa
Website: www.zantel.com

KUHUSU ZANTEL
Mtandao wa Mawasiliano wa Zanzibar (Zantel) ni wa kipekee kwa mawasiliano nchini Tanzania unaofungua milango kwa huduma za kimataiafa za simu na data kupitia huduma zake za CDMA, GSM, 3G  na 4G.
Zantel imekuwa ikihudumia wateja wake kwa ubora na huduma ya haraka ya intaneti yenye kasi nchini Tanznia.
Zantel imepokea tuzo mbalimbali kutokana na kutambuliwa kutoa huduma bora na ufumbuzi kwenye sekta ya mawasiliano. Baadhi yake ni pamoja na Tuzo ya GSMA M – Health. Zantel imedhamiria kuwaunganisha watu ulimwenguni ili wawe mstari wa mbele kupata tarifa kwa haraka.
Kwa maelezo zaidi tafadhali, tembelea mtandao wetu…www.zantel.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.