Habari za Punde

Polisi wamshikilia mmoja baada ya shambulizi la kisu


JESHI la Polisi mkoa wa Mjini Magharib Unguja, linamshikilia Khamis Mohamed Pili (38) mkaazi wa Mtoni baada ya kumshambulia mwenzake kwa kumpiga kisu cha ubavu wa kushoto baada ya kutokea sintofahamu kati ya wawili hao.
 Kamishna Msaidini wa Polisi ambae pia ni Mkuu wa Utawala na Raslimali watu kutoka Polisi Madema, Haji Abdalla Haji, alisema tukio hilo lilitokea  Oktoba 20 mwaka huu, majira ya saa 1:10 usiku.
 Alisema mbali ya sehemu hiyo pia mtuhumiwa alimjeruhi majeruhi huyo katika sehemu ya kichwa, kifua na mguu wa kushoto.
 Alisema mtuhumiwa huyo ambae ni ndugu wa majeruhi huyo alimshambulia kisu mara baada ya kutokea sintofahamu kati ya wawili hao ingawa chanzo cha ugomvi huo hakijafahamika.
Aidha alisema kuhusiana na tukio hilo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha tukio hilo ili mtuhumiwa achukuliwe hatua za kisheria.
 Alisema baada ya tukio hilo majeruhi alikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja  kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
 Alisema mtuhumiwa wa tukio hilo yuko ndani na anaendelea kuhojiwa kujua chanzo na sababu ya kutekeleza unyama huo kwa mwenzake.
 Hata hivyo, alisema mtuhumiwa atachukuliwa hatua kali  kwa kujaribu kutaka kufanya mauaji na pia aliwataka vijana kutochukua hatua mikononi pale unapotokezea ugomvi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.