Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Awaapisha Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar na Viongozi Wengine Ikulu leo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Khamis Ramadhan Abdala kuwa Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bibi Aziza Iddi Suwedi kuwa  Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Kubingwa Mashaka Simba  kuwa  Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha  Bw.George Joseph Kazi kuwa  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla alikuwa Mrajis wa Mahkama Kuu ya Zanzibar
Baadhi ya Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar ni miongoni mwa Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kiapo cha Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar walioapishwa leo na Viongozi wengine kazi iliyofanya na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar  leo,(kutoka kulia)Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi,Kadhi Mkuu wa Zanzibar  Sheikh Khamis Haji na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Katiba, Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Khamis Juma Maalim
Majaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar wakipitia hati zao za viapo kabla ya kuapishwa Rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) kushika wadhifa walioteuliwa hafla ya kiapo ilifanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 02/10/2017.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.