Taarifa kwa Vyombo vya Habari.
Kwa mujibu
wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu cha 4 (a) cha Sheria ya Usajili ya Magazeti
na Vijarida Namba 5 ya Mwaka 1988, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, amemteua Bwana Yussuf Omar Chunda kuwa
MWENYEKITI WA BODI YA USHAURI YA USAJILI WA MAGAZETI NA VIJARIDA, ZANZIBAR.
Uteuzi huo
umeanza tarehe 19 Oktoba, 2017.
Taarifa ya
uteuzi huu kutoka Ikulu Zanzibar, imesainiwa na Dkt. Abdulhamid Y. Mzee, Katibu
wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment