Mratibu wa Mauzo na Masoko wa Zantel-Zanzibar, Ndg. Haji Said Khatibu (katikati) akimsaidia Mkazi wa kijiji cha Uroa, Mkoani Kusini-Unguja, Bi. Fatma Abbas kuvuna zao la mwani baada ya Kampuni ya Zantel kuwatembelea baadhi ya wakulima walionufaika na msaada wa Tsh milioni 10 zilizotolewa mwaka jana kwa ajili ya kuwaendeleza wakulima hao. Kushoto ni mkazi wa mjini Unguja-Zanzibar Issa Yusuf.
Watu wengi waliopo nje ya Zanzibar wanadhani
kuwa Unguja na Pemba ni visiwa vyastarehe na mahali pa kupumzika tu. Uzuri wa Zanzibar
umekuwa kivutio kwa watalii kutoka nchi mbalimbaliduniani jambo ambalo
linaifanya Zanzibarkuimarika kwenye masuala ya Utaliii.
Hata hivyo ukija kwenye masuala ya
Kilimo, watu wengi wamekuwa wakiamini kwamba Utalii na kilimo cha karafuu ndio
mambo pekee ya kibiashara yanayofanyika visiwani humo.
Kilimo cha zao la ‘MWANI’kimekuwa ni
miongoni mwa mazao makubwa ya biasharayanayouzwa nje ya nchi tangu mwanzoni mwa
miaka ya 1990.
Shughuli za kilimo cha zao la mwani zilianza
Zanzibar mwaka 1989 na zao hilo limewavuta watu wengi kujishugulisha na
biashara hiyo licha ya kuwapo kwa changamotokadhaa wanazokabiliana nazo.
Takribani asilimia 80 ya wanawake
Zanzibar wanajishughulisha na kilimo cha zao hilo na wamekuwa wakitoa wito kwa
Serikali na Taasisi za watu binafsi kuwasaidia katika kutatua changamoto
mbalimbali zinazowakabili.
Juni mwaka 2016, kampuni ya
mawasiliano inayoongoza katika huduma ya intaneti ya Zantel ilikubali
kushirikiana na wakulima baada ya kutoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa Jumuiya
ya Wakulima wa Mwani Zanzibar (JUWAMWANZA) ili kuwawezesha wanachama hao
kununua vifaa vya kilimo hicho ikiwamo kamba navijiti (pegs) ambavyo vilisambazwa
kwa wakulima wa mwani katika vijiji 83 vilivyopokatika mwambao wa pwani ya
Unguja, jambo lililofanikisha kilimo cha zao hilo kuendelea kufanya vizuri.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed
Baucha alisema Kampuni hiyo ya Mawasiliano imefurahishwa kupata mrejesho kuwa
msaada walioutoa umeleta mafanikio kwa wakulima wa mwani na kuwaahidi kuendelea
kushirikiana na wakulima hao ili kuwasaidia kufanya kilimo cha kisasa na kuongeza
uzalishaji zaidi.
Katika mahojiano ya hivi karibuni
mjini Zanzibar, Baucha alisema, “Mwaka huu Zantel inasherehekea miaka miwili tangu
Millicom ilipoichukua kutoka kwa Kampuni ya Etisalat ya Falme za Nchi za
Kiarabu (UAE). Hivyo msaada wetu wa mwaka jana ulikuwa chini ya mradi wa wetu
wa Uwajibikaji kwa jamii katika maeneo ambayo tunafanya shughuli zetu na hivyo
tuliamua kuwasaidia wanawake ambao wawamejikita kwenye kilimo cha zao la mwani
kisiwani hapa.”
Baucha alisema chini ya Millicom, miradi
ya Zantel inayosimamiwa na Idara ya Uwajibikaji kwa jamii imejikita kuwasaidia
wajasiriamali, makundi maalumu kama vile walemavu, vijana, pia Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano sambamba na kuwainua wanawake katika kuleta maendeleo
katika jamii na taifa kwa ujumla.
Alisema Zantel kuwasaidia wakulima wa
zao la mwani, pamoja na kuitikia wito wa serikali baada ya kuziomba sekta
binafsi kuunga mkono juhudi za wakulima 23,354 wa zao la mwani Zanzibar
kuhakikisha kwamba wanauza mazao yao na kuongezea thamani.
Kiongozi huyo wa Zantel Zanzibar
aliongeza kwamba kampuni hiyo ipotayari kuwasaidia wakulima wa mwani katika
nyanja ya mafunzo ili kuwa na ujuzi zaidi kwa kilimo cha kisasa kwa kutumia
intaneti ya Zantel kwa kujifunza zaidi kuhusu wakulima wengine wa mwani wa maeneo
mengine duniani kujua nini wanachokifanya.
Licha ya kuwapa mafunzo ya jinsi yakutumia
intaneti, Zantel itawapa pia elimu ya kutumia huduma ya EzypESA ili kutunza
fedha zao na wakati mwingine kuhamisha fedha zao kutoka benki kwenda kwenye
mtandao wa Zantel au kwenda kwenye akaunti zao za benki pindi wanapovuna na
kuuza mazao yao.
“Tunataka kuwarahishia maisha na
kufanyaia wepesi kwa kuhakikisha wanapata muda mwingi zaidi kwenye kazi zao za uzalishaji
wa zao hilo ili waweze kuongeza mauzo badala ya kutumia muda mwingi kwenda
mjini kufanya miamala au kukaa kwenye foleni kwa muda mrefu wakisubiri kulipia
malipo ya huduma mbalimbali,” aliongeza.
Chini ya umoja wao wa Jumuiya ya
Wakulima wa Mwani Zanzibar, imekuwa rahisi kwa Zantel kuwasaidia jambo ambalo
wanakiri kwamba limekuwa na manufaa kwao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa
JUWAMWAZA, Pavu Mcha Khamis alisema, “Msaada wa Zantel daima utakumbukwa
kutokana na kusaidia vijiji 48 Unguja na maeneo mengine ya Kisiwa cha Pemba.
Alisema wakulima wa mwani wanahitaji
vifaa mbalimbali hivyo wanaendelea kutoa wa witokwa Serikali na wadau wengine
wanaoitakia mema sekta hiyo kuendelea kuwasaidia wakulima wa zao la mwani.
Pavu alifafanua kwamba wakulima wengi
ambao wameelekeza nguvu zao kwenye kilimo cha mwani wanakabiliwa na kutokuwa na
ujuzi kwenye kazi hiyo, uhaba wa vifaa ikiwamo viatu vya mpira, Kamba, vijiti
na bei ndogo ya zao hilo sokoni vitu ambavyo viliisukumaKampuni ya Zantel kuwa
mstari wa mbele katika kutatua baadhi ya changamoto hizo kwa kushirikiana na wanunuzi pamoja na
serikali.
Kwa mujibu wa Pavu, Mwani aina ya
Cottoni na Spinosum ndivyo vinastawi kwa wingi Zanzibar na kuna takribani
makampuni saba ambayo hununua mwani kutoka kwa wakulima kisiwani humo lakini zaidi
Makampuni hayo hununua Spinosum ambayo ndiyo huwa inauzwa pia nje ya nchi.
Alisema kwa kawaida mwani aina ya
spinosum huchukua takriban siku 45 na 60 kukua hadi kuvuna na ndio unapatikana
kwa wingi kwa sababu mwani aina ya Cottonii unauzwa bei ghali na wakati
mwingine mwani huo hukabiliwa na hali mbaya ya mabadiliko ya hewa.
Katika mahojiano ya hivi karibuni na
wakulima wa mwani wakielezea jinsi ambavyo wamenufaika na shilingi 10 milioni zilizotolewa
na Zantel, Mjane Sharifa Thabit (51) wa
Kijiji cha Pongwe kilichopo, kilometa 43 toka Unguja Kusini, amekuwa akilima zao hilo tangu lianze kulimwa
Zanzibar zaidi ya mongoni mitatu iliyopita, alieleza jinsi ambavyo amefanikiwa
kwenye kilimo hicho.
Alisema kwamba vifaa vya kilimo
ambavyo vilitolewa na ZantelJuni mwaka jana, vimekuwa msaada mkubwa kwenye
shughuli hiyo ya kilimo.
“Tunaishukuru Zantel kwa msaada wao
na tunawaomba waendelee kutusaidia. Mipango yetu ni kupata mafunzo kuhusu
kilimo cha kisasa cha mwani,” alisema.
Mkulima mwingine wa kijiji cha jirani
cha Uroa ambaye anafanya shughuli ya kilimo kama hicho, Fatma Abbasi anasema
huwa anavuna mazao yake na kwenda kuyakaushia nyumbani.
“Hii kazi ni ngumu sana lakini
tunahitajika kuifanya ili kuendesha maisha,” alisema
Alipoulizwa ni kwa namna gani
alinufaika na Shilingi milioni 10 zilizotolewa na Zantel, Alisema “ Ninashukuru
sana kuwa sehemu ya watu walionufaika na msaada ule mwaka jana. Imenisaidia
sana kutuinua sisi wakulima.”
Alisema baada ya msaada huo wakulima
wengi waliweza kuongeza kipato chao jambo lililowawezesha kuongeza uzalishaji
na kwa upande wake alifanikiwa kujipatia kati ya shilingi 300,000 na 400,000
wakati wa mavuno ya kwanza.
Pongwe na Uroa ndio vijiji vyenye
idadi kubwa zaidi ya watu wanaojishughulisha na kilimo cha mwani katika maeneo
ya Visiwa vya Unguja na Pemba lakini bado wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
za vifaa vya kilimo na bei ndogo yazao hilo.
Zanzibar huuza takriban tani 12,000 za
mwani nje ya nchi kila mwaka ikiwa ni ya tatu kwa uuzaji wa mwani duniani ikiwa
nyuma ya Phillipines inayoongoza naIndonesia.Zanzibar imeendelea kupata
changamoto kubwa ya Soko kutokana na ushindani kutoka kwenye nchi kama Philippines.
Kwa mujibu wa wakulima wanaweza
kuzalisha bidhaa zaidi ya 50 kutokana na zao la mwani ikiwamo juisi, dawa za
hospitali, vipodozi na vingine vingi zaidi huku nchi za nje wakitumia mwani kama
mbolea.
Maeneo mengi ambako hutumia zao hilo
kama chakula ni barani Asia hasa nchi za
Japani, Korea na China ambako kilimo cha mwani kimekuwa muhimu katika kuinua
Uchumi wa viwanda.
No comments:
Post a Comment