Habari za Punde

MZEE ZAM AULA CECAFA

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Makamo wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA Unguja) Mzee Zam Ali ameteuliwa kuwa mjumbe katika kamati itakayosimamia Mashindano ya Chalenji CUP yaliyoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Mashindano ambayo yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya.

CECAFA wamemteuwa Mzee Zam kwakuwa ni mzowefu katika Mashindano hayo ambapo ni Mzanzibar pekee kwenye kamati hiyo.

Wengine waliochaguliwa katika kamati hiyo ni Mutasim Gafar (Sudan), Abdigaan Arab Said (Somalia), Jacob Odundo (Kenya), Ashinafi Ejigu (Ethiopia), Aimable Habimana (Burundi), Rogers Byamukama (Uganda), Ajong Domasio Ajong (Sudan ya Kusini) na Ahmed Mgoyi (Tanzania Bara).

Wengine ni Sunday Kayuni (Tanzania Bara), Mossi Yussuf (Burundi), Celestine Ntangugira (Rwanda), Yigzaw Ambaw (Ethiopia), Bernard Mfubusa (Burundi), Maxim Itur (Kenya), Rogers Mulindwa (Uganda), Bonny Mugabe (Rwanda), Gishinga Njoroge (Kenya), Amir Hassan (Somalia) na Nicholas Musonye (Kenya).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.