Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kesho Jumatano inatarajia kucheza mchezo wa kirafiki na klabu ya Taifa ya Jang’ombe pambano litakalopigwa majira ya saa 2:00 za usiku katika uwanja wa Amaan.
Zanzibar Heroes inajiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya ambapo wamepangwa kundi A pamoja na ndugu zao Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya.
No comments:
Post a Comment