Habari za Punde

Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara huenda wakaachwa Zanzibar Heroes baada ya klabu zao kuwabaniaNa Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), ambao wanacheza ligi kuu soka Tanzania bara huenda waachwa katika kikosi hicho kutokana na kutopewa ruhusa na vilabu vyao kujiunga na timu hiyo ya Taifa mpaka ligi kuu bara itakapokwenda mapumziko.

Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Morocco) amesema kutokana na kutopewa ruhusa wachezaji hao huenda wakawasamehe na badala yake wakawachagua wachezaji wengine wanaocheza soka hapa hapa Zanzibar.

Morocco amesema ikifika Novemba 15 ikiwa bado wachezaji hao hawajawasili kambi ya Heroes watalazimika kuwaacha na kuongeza nguvu kwa vijana wanaocheza vilabu vya Zanzibar kwani hawawezi kuwaruhusu wachezaji hao kujiunga na kambi siku chache kabla hawajasafiri.

"Tumeshaanza mazoezi tangu juzi, lakini uhakika wa kuwapata wachezaji wanaocheza ligi ya bara ngumu, tumewasiliana na vilabu vyao lakini wametuambia wachezaji hawaruhusu kujiunga na sisi mpaka ligi isimame Novemba 19, nasisi tunataka kuondoka Novemba 22, sasa itakuwa muda hawajapata kukaa na wenzao kwasababu pengine wafike Zenj Novemba 20 au 21 sasa apo bora tuwasamehe na tuwaite wengine wanaocheza hapa hapa Zanzibar". Alisema Morocco.

Wachezaji waliyoitwa awali katika kikosi cha Zanzibar Heroes ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) na Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji) pamoja na washambuliaji Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga) na Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli).

Wakati huo huo Mlinzi kinda wa Zanzibar Heroes aliyeitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho Ibrahim Abdallah wa Taifa ya Jang’ombe amepania kupigana kufa kupona ili apate nafasi ya kwenda nchini Kenya katika Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.