Habari za Punde

Harambee Stars waahidiwa kila mchezaji Sh Milioni 4 wakiifunga Zanzibar Heroes

Na Mwandishi wetu

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars wameahidiwa kila mchezaji kupewa kiasi cha Laki mbili za Kenya ambazo ni sawa na Sh Milioni 4 kwa kila mchezaji endapo itaibuka washindi dhidi ya Zanzibar Heroes katika mchezo wa fainali unaotarajiwa klufanyika kesho katika Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos nchini Kenya.

Chama cha Mpira cha Kenya, Football Kenya Federation kimetoa ahadi hiyo kupitia mwenyekiti wake Nick Mwenda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huku akisema wametenga kiasi cha Sh Milioni sita za Kikenya kwa ajili ya zawadi kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi

Wakati huo huo magazeti ya Kenya katika kuonesha kuingiwa na kiwewe na woga kuikabili Zanzibar Heroes wameanza kuingiza Imani za kichawi na kishirikana baada ya kuwashuku Zanzibar kwamba kila kila wakianza mpira mwanzo wa mchezo basi pasi yao ya pili lazima ipigwe nje ya uwanja kwa mujibu wa kamati yao ya ufundi ilivyowaagiza

Hata hivyo kiungo mahiri wa Zanzibar Heroes, Mchezaji wa Mtibwa Sugar, Mohammed Issa 'Banka' amepuuzia habari hizi na kusema ni ari na umoja wa timu ndio vitu pekee vilivyowasaidia kwani kwa Zanzibar Heroes kucheza michezo ya CECAFA ni kama kupanda ndege kwenda Urusi kucheza Kombe la Dunia.


Banka alizidi kusisitiza: ‘Zanzibar ni nchi ndogo sana na wengi wetu ni maskini hivyo CECAFA kwetu ni kama World Cup hivyo ni sehemu pekee kwetu kucheza kwa kiwango cha hali ya juu si uchawi jamani’ Alimalizia Mohammed Issa ‘Banka’

Tayari Baraza la Wawakilishi limetoa ahadi ya kuwazawadia Zanzibar Heroes Sh Milioni kumi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed akisistiza ahadi yake ya kuwapongeza na kuwazawadia Heroes ipo palepale.


Akizungumza na Waandishi wa habari kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma amesema kutokana na hatua iliyofikia timu hiyo kwa jitihada waliyoiyonesha  vijana hao katika michuano hiyo  Dk. Shein chini ya serikali yake ameahidi kuwapa zawadi vijana wa Zanzibar Heroes  pindi watakapo rejea Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.