Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud
Sururu (kati kati), akiwatoa hofu Watendaji wa Mamalaka ya Vitambulisho vya
TAifa (NIDA) kwamba kuanzia mwezi January 2018, Idara ya Uhamiaji Zanzbar imejipanga
kushughulikia maombi ya Vitambulisho vya Taifa kwa Raia wote watakaofika katika
Ofisi yao iliyopo Kinduni, Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja, badala ya kufuata
huduma Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini iliyopo Kivunge. Hatua hiyo ni
utekelezaji wa Ahadi za Serikali kufikisha huduma karibu na Wananchi. Aliyasema
hayo wakati alipotembelea Ofisi hizo wakati wa ziara ya kikazi katika Wilayani
humo tarehe 05 - 06 Disemba, 2017
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu, akiambatana
na Maafisa Waandamizi wa Uhamiaji wakitembelea maeneo mbalimbali yanayotumiwa
na Wahamiaji wasiofata Sheria katika ukanda wa Pwani za Kiwengwa, Pwani
mchangani, Matemwe, Pongwe, Kendwa na Nungwi, wakati alipofanya ziara ya kikazi katika maeneo yote yanayofanyiwa
kazi na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu
(kati kati), akielezea jinsi Idara ya Uhamiaji inavyopiga hatua katika kutatua
changamoto ya ufinyu wa Ofisi na Vitendea kazi katika Wilaya zote Unguja na
Pemba, ambapo alisema hivi karibuni Idara yake inatarajia kupokea magari (12)
na Pikipiki (20) ambazo kwa kiasi kikubwa zitakidhi uhaba uliopo. Aliyasema
hayo wakati wa ziara ya kikazi kwenye maeneo mbali mbali Mkoa wa Kaskazini
Unguja tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Haroub Iddi Juma, akitoa ufafanuzi
kwa Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu juu ya Ramani ya
Kiwanja kilichopo kijiji cha Gamba, Wilayani ya Kaskazini “B” wakati
alipotembelea kiwanja hicho jana tarehe 05 Disemba, 2017 kinachotarajiwa
kujengwa Ofisi ya Uhamiaji Wilayani humo.
Sheha wa Shehia ya Moga Bwana Juma Kombo Juma (kati
kati), akimuonesha Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu mipaka
ya Kiwanja kilichopo Shehia ya Gamba, Wilaya ya Kaskazini “B” kinachomilikiwa
na Idara ya Uhamiaji. Hizo ni juhudi za Idara hiyo kufikisha huduma zake karibu
na wananchi kwa kujenga Ofisi na Makaazi ya Askari katika Ofisi za Mikoa na
Wilaya zote zilizopo Zanzibar.
Sheha wa Shehia ya Kiwengwa Bwana Maulid Masoud Ame, akimuleza
Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu na Maafisa waandamizi wa
Idara hiyo alioambatana, changamoto za wageni katika maeneo yao. Wakat wa ziara
ya kikazi kujionea utendaji kazi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja
na Wilaya zake tarehe 05 - 06 Disemba, 2017.
No comments:
Post a Comment