Habari za Punde

Kila la Kheri Zanzibar Heroes


Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo inaingia dimbani kupambana na wenyeji Kenya katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea nchini Kenya.

Blog ya ZanziNews inaitakia kila la kheri timu yetu ili na leo iibuke na ushindi kama ilivyoweza kushinda katika michezo miwili iliyopita na kujiweka katika mazingira mazuri ya kucheza nusu fainali.

Ikumbukwe kwamba Timu yetu imeweza kushiriki katika mashindano haya licha ya kuwa na maandalizi duni, kwani hata safari ya kwenda nchini Kenya ilikuwa ni ya kuungaunga tu kwa usafiri wa mabasi hadi kuwasili Machakos.

Hata hivyo ari kubwa waliyoonesha vijana wetu licha ya changamoto, licha ya kutokuwa na majina makubwa lakini soka wanalitendea haki kwa uthibitisho wa michezo yote waliyoibuka washindi hawakubahatisha bali walistahiki.

Na leo macho yetu  yatakuwa mjini Machakos kuitakia ushindi mwengine dhidi ya miamba ya Harambee stars kwani wazungu wana msemo The bigger they are, The harder they fall.

Tuiombee dua kwa wingi timu yetu iibuke na ushindi leo

Go Zanzibar Heroes Go!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.