Habari za Punde

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja afanya ziara ya kushtukiza Wilayani na kujionea madudu
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Mheshmiwa Idrissa Kitwana Mustafa afanya ziara ya kushtukiza sehemu Mbali Mbali ndani ya Wilaya ya Kusini usiku wa kuamkia leo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alifika Kizimkazi Mkunguni na kujionea Vijana kadhaa wakitokea mjini na wengine ni wanafunzi wakiwa kwenye sherehe ya "Day Out" huku wakicheza Mziki tena kinyume na utaratibu.

Mheshmiwa Idrissa alifika pia hoteli inayoitwa "Before" Iliyopo Paje na kushuhudia Mziki ukipigwa kinyume na utaratibu.

Aidha alitembelea kijiji Cha Bwejuu kwenye hoteli inayoitwa "Kwa Lila" na kushuhudia pia Mziki ukipigwa kinyume na utaratibu.

Mkuu huyo wa Wilaya alifanya pia ziara kwa watu wanaosadikiwa kuuza pombe ya kienyeji na kufanikiwa kukuta pombe aina ya "Bombonya".

Watu kadhaa waliokutwa na makosa Mbali Mbali kwenye ziara hiyo wapo chini ya ulinzi wa Jeshi la  Polisi Wilaya ya Kusini Unguja kwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.