Habari za Punde

MSAMA AMSHUKURU RAIS DKT. MAGUFULI KWA UAMUZI WA KUWASAMEHE WASANII BABU SEYA NA PAPII KOCHA

Na Kajunason/MMG.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Action Mart, Alex Msama amshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kitendo cha kutoa msamaha kwa wanamuziki maarufu nchini, Papii Nguza (Papii Kocha) na baba yake mzazi, Nguza Viking (Babu Seya) aliyekuwa akitumikia kifungo cha maisha katika gereza la Keko jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaama, Msama ambaye ni alikuwa ni mjumbe wa Bodi wa BASATA na mpigania haki zawasanii na vile vile ni mlezi wa wasanii mbali mbali amesema jambo alilolifanya ni jema sana na ametekeleza maagizo ya Mungu ambayo anatushauri tusamehe. "Ukisoma hata kwenye vitabu vya biblia suala la kusamehe alishalisema, katika Mathayo 18:21-22...

Ndipo Petro akamjia Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je, hata mara saba?” Yesu akamjibu, ''Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.' alisema Msama. Msama aliongeza kuwa jambo hilo ni kubwa na halina kipingamizi chochote maana kila kona ya Tanzania maamuzi hayo yamepokelewa kwa mikono miwili.

Aliongeza kuwa wafanyabiashara wote wanaofanya kazi za sanaa ni vyema wakafuata taratibu kwa kuuza kazi halali zilizo na stika za TRA ambazo zitawanufaisha wasanii na serikali kwa ujumla. Hata hivyo, zoezi laukamataji Kazi feki za sanaa litaendelea katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni zoezi la nchi nzima.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.