Habari za Punde

Uganda Cranes v Zanzibar Heroes katika Picha Wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes  Feisal Salum na Mudathir Yahya wakishereheka baada ya kiungo Mohammed Issa 'Banka'  (jezi na 10) kuwafungia bao la pili la ushindi lililoizamisha Uganda Cranes
 Wachezaji wa Timu ya Zanzibar Heroes wakisujudu Sijda ya Shukrani  kwa Mola wao baada ya kuwatunga Waganda goli la pili la ushindi lililofungwa kwa njia ya Penelti na Mohammed Issa 'Banka'
Kungo wa Uganda Allan Kaymbadde akifanya maarifa kumpita beki wa Zanzibar Heroes, Abdallah Salum katika mchezo wa Nusu Fainali ya Cecafa. Zanzibar Heroes imeshinda 2-1 na kuingia fainali ambapo itapambana na Harambee Stars ya Kenya

 Mshambuliaji wa Timu ya Zanzibar Heroes, Suleiman Kassim 'Seleembe' akiumiliki mpra dhidi ya mlinzi wa timu ya Uganda Cranes, Bernard Muwanga wakati timu hizi zilipokutana katika nusu fainali ya kombe la CECAFA. Zanzibar ilishinda Uganda 2-1
Winga wa Uganda Cranes, Allan Katterega akijaribu kumpita kiungo wa Zanzibar Heroes, Mudathir Yahya wakati timu hizi zilipokutana katika nusu fainali ya kombe la CECAFA. Zanzibar ilishinda Uganda 2-1

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.