Habari za Punde

Rais Dk Shein, Ahutubia Katika Kilele Cha Maadhimisho ya Serehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar Katika Uwanja wa Amaan Znzibar leo.12-1-2018.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Wananchi wa Mikoa Mitano ya Zanzibar wakati wa hafla ya Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. na Kuhudhuriwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Marais Wastaaf wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, Mzee Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dkt. Amani Karume na Makamu wa Rais Mstaaf wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyama Vya Siasa Tanzania.


 Baadhi ya Mabalozi Wanaoziwakilisha Nchi Zao Nchini Tanzania wakifuatilia Sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Viwanja vya Amaan Zanzibar.
Wananchi wakishangilia wakati wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia hadhara hiyo, ya kuadhimisha Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.




 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mstahiki Meya wa Mji wa Zanzibar Mhe. Khatib Abdurahaman Khatib baada ya kumaliza kuhutubia katika hafla ya maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud baada ya kumalizika hafla ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Amaan Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.