Habari za Punde

Tangazo Kwa Umma

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIATANGAZO KWA UMMA

Kamati ya Uteuzi wa Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, iliyoundwa na Ibara ya 129(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inautangazia umma kwamba, Waombaji wa Kazi katika nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaliyopitishwa na Kamati kwa madhumuni ya kusailiwa yametolewa katika Magazeti ya Habari Leo, Daily News, na Zanzibar Leo ya tarehe 17 na 18 Januari 2018, pia kwenye tovuti ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora – http://www.chragg.go.tz

Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 7 ya Kanuni za Uteuzi wa Makamishna za Mwaka 2001, Kamati ya Uteuzi inawaomba wananchi kwa ujumla kuwasilisha maoni yao kuhusu sifa na uwezo wa Waombaji waliopitishwa na Kamati. Inasisitizwa kuwa maoni ya wananchi yatashughulikiwa na Kamati kwa njia ya siri.

Siku ya mwisho ya kupokea maoni ya wananchi itakuwa ni tarehe 23 Januari, 2018. 

Maoni hayo yawasilishwe kwa njia ya maandishi kwa:

Katibu,

Kamati ya Uteuzi,

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

Kivukoni Front, (Karibu na Mahakama Kuu ya Tanzania),

S.L.P 9050, DAR ES SALAAM.

Au kwa mkono:

Katibu Mtendaji,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Mtaa wa Luthuli, Jengo la Haki Na. 10,
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM.
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz

KATIBU

KAMATI YA UTEUZI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.