Habari za Punde

Yanga African Yaibuka na Ushindi Kombe la Mapinduzi Yaifunga Timu ya Mlandege 2-1 Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Kikosi cha Timu ya Yanga African kilichotoka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Timu ya Mlandege katika mchezo wake wa kwanza wa Michuani ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Bao la kwanza la Yanga limefungwa katika dakika ya 7na 36 ya mchezo huo kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji wake Juma Mahadhi. Bao la kufutia machozi la Timu ya Mlandege limefungwa na mshambuliaji wake Omar Makamekatika kipindi cha pili cha mchezo huo katika dakika ya 48. Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Yanga African imetoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 2-1.   
Kikosi cha Timu ya Mlandege wakisoma dua kabla ya kuazi kwa mchezo wao wa Kombe la Mapinduzi na Timu ya Yanga African mchezo uliofanyika jana usiku,2/1/2018. katika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Mshambuliaji wa Timu Yanga Juma Mahadhi akishangilia bao lake la Pili alililofunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.


Wachezaji wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la kwanza lililofunguwa na mshambuliaji Omar Makame katika dakika ya 48 ya mchezo huo kipindi cha pili. 
Wachezaji wa Timu ya Mlandege wakishangilia bao lao la kwanza lililofunguwa na mshambuliaji Omar Makame katika dakika ya 48 ya mchezo huo kipindi cha pili. 


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.