Habari za Punde

ZAHA kufanya uchaguzi Februari 18


 
Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Chama cha Mpira wa mikono Zanzibar (ZAHA) kitafanya Uchaguzi wake ambao unatarajiwa kufanyika February 18, 2018.
Akizugumza na Mtandao huu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Said Ali Mansabu amewataka wadau mbali mbali wa michezo kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kugombea nafasi tofauti kwenye chama hicho.
Amesema baadhi ya wadau wanapenda kuwalaumu viongozi hivyo hiyo ni fursa kwao kuja kugombea nafasi katika chama chama hicho.
“Mimi nawaomba wanamichezo wenzangu hasa wale wanoumwa na Handa ball, wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu katika chama hichi ili kupunguza yale malalamiko ambayo watu wanasema viongozi wana matatizo wa chama hichi basi hii ni fursa ya kupata viongozi wapya”. Alisema Mansabu.
Viongozi wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo watakaa madarakani kuanzia mwaka 2018 hadi 2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.