Habari za Punde

Fahamu Makundi Mbalimbali ya Magonjwa ya Mbwa - Sehemu ya Kwanza

Picha na Josephat Lukaza
Na Josephat Lukaza - Dog Tips Tanzania
Mbwa ni mnyama kama wanyama wengine na pindi unapofikiria kufuga mbwa basi kwanza Jiulize Maswali yafuatayo. Moja Upo tayari kumuhudumia mbwa wako kwenye Chakula, Maradhi, Matibabu, Mafunzo na Kutoa Muda wako wa angalau kuanzia nusu saa  mpaka masaa mawili kwaajili ya kukaa nae, kucheza nae na uangalizi? Kama jibu ni HAPANA basi fahamu kuwa hujafikia hatua ya kufuga Mbwa ni heri uache maana vinginevyo yatakuwa mateso kwako na kwa mbwa mwenyewe. Mbwa anahitaji upendo kama ambavyo Binadamu tunavyowapenda binadamu wenzetu na hata kuwahudumia pale wanapokuwa wagonjwa basi na Mbwa ni hivyo hivyo unapoamua kufuga mbwa fahamu ya kuwa naye  ni mnyama kama mnyama mwingine ambapo akiumwa anahitaji matibabu. Leo tutaangalia Makundi mbalimbali ya Mangonjwa yanayoweza kumshambulia mbwa, mnyama anayekaribia uhusiano na mbwa, na hata binadamu pia.
Leo tutaangazia Makundi Mawili tu huku Makundi mengine yataangaziwa Katika post zetu zijazo kikubwa ni endelea kufuatilia post zetu kupitia Hapa DOG TIPS TANZANIA ili upate ufahamu na kuweza kutunza vizuri mbwa wako. Kuna aina nyingi ya magonjwa ya mbwa na magonjwa hayo tutayafahamu kupitia katika makundi haya mbalimbali. Makundi hayo Mawilin ni kama yafuatavyo
1: VIRAL INFECTIONS
Viral infections ni magonjwa yanayosababishwa na virusi kutoka kwa mnyama mmoja kwenda kwa mnyama mwingine ambapo magonjwa haya yapo mahususi kwaajili ya mbwa na hata binadamu. Katika Kundi hili la Viral kwa mbwa kuna magonjwa kama vile Rabies (Kichaa cha Mbwa), Canine parvovirus ,Canine coronavirus, Canine distemper ,Canine influenza, Infectious canine hepatitis , Canine herpesvirus , Pseudorabies na Canine minute virus Haya ni baadhi tu ya magonjwa ambayo ni kwaajili ya mbwa lakini pia yapo ambayo yanaweza kumdhuru binadamu pia kama hatochukua tahadhari mapema. >>>  SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.