Habari za Punde

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Awasili Mkoani Mwanza Kuaza Ziara Yake ya Kiserikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili Jijini Mwanza jioni hii na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, na Viongozi wengini wa Mkoa huo.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika Uwana wa Ndege Mwanza kuaza ziara yake ya Kiserikali Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mwanza alipowasili katika Uwana wa Ndege Mwanza kuaza ziara yake ya Kiserikali Mkoani humo.
Makamu wa Rais anategemewa kuanza ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kesho mkoani Simiyu.
Katika ziara hiyo itakayoanza kesho tarehe 19/2/2018 na kumalizika tarehe 22/2/2018, Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa mradi  wa maji Kiloleli na kuweka jiwe la msingi na baada ya hapo atazungumza na wanachi Lamadi .
Pia Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za viongozi wa mkoa  katika eneo la Nyaumata.
Miradi mingine ambayo Makamu wa Rais ataitembelea ni Kukagua Ujenzi wa Barabara za Lami Bariadi mjini chini ya Programu ya uimarishaji wa Serikali za Mitaa za Mjini.
Makamu wa Rais atakagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Mwanjoro na kusalimia wananchi siku ya tarehe 20, pia atasalimia wananchi wa Mwanhuzi Mjini, Mwandoya (Meatu)
Tarehe 21, Makamu wa Rais atafungua Kongamano la Elimu ya Juu na Uchumi wa Viwanda Tanzania kasha atafungua jengo la Utawala la halmashauri ya Itilima na kusalimia wananchi, kufungua jingo la upasuaji  la Samia Suluhu  Hassan katika Hospitali ya Wilaya  ya Maswa na kuzungumza na wananchi katika viwanja vya nguzo nane.
Siku ya tarehe 22, Makamu wa Rais ataongoza Mahafali  ya 34 ya Chuo Kikuu Huria .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.