Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi Leo.

Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba Mhe. Omar Seif Abeid akichangia na kuuliza swali wakati wa mkutano wa Baraza la Wawakilishi unaofanyika katika Ukumbi wa jengo la Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar
Mwakilishi wa Jimbo la Chakechake Pemba Mhe.Suleiman Sarahan Said kushoto akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Kuteuliwa Mhe Ahmada wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Zanzibar.
Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake Mhe.Salha Muhammed Mwinjuma akifuatilia michango inayowakilishwa na wajumbe wa Baraza wakichangia mswada wa Sheria
Mwakilishi wa Jimbo la Donge Zanzibar na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt,Khalid Salum Mohammed kushoto akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Kuteuliwa Mhe.Mohammed Aboud Mohammed, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Baraza Chukwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe Khamis Juma Maalim akijibu maswali yalioulizwa ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi   linaloendelea Chukwani Mjini Zanzibar.

Naibu Waziri Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto  Mhe,Shadya Mohammed Suleiman akijibu maswali yalioulizwa ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  linaloendelea Chukwani Mjini Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai - Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.