Habari za Punde

Mtumishi wa CCM Zanzibar afariki dunia

                 SALAMU ZA RAMBI RAMBI

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Mtumishi wa Chama Marehemu  Bw. Maulid Sleyum Said aliyefariki Februari 16 ,2018.
Bw.Maulid amefariki dunia akiwa katika hospitali ya Global iliyopo Vuga Mjini Zanzibar alipokuwa akipatiwa matibabu  baada ya kuugua ghafla.
Katika Salamu zake  Dk. Mabodi amesema  CCM imepokea taarifa ya kifo cha mtumishi huyo  kwa Mshutuko, Majonzi na uzuni  kubwa, kwani Marehemu enzi za uhai wake alikuwa Mwadilifu aliyefanya kazi kwa bidii  katika utumishi wake kwa muda wote wa uhai wake.
Pamoja na hayo ametoa pole kwa Wanachama, Viongozi na Watendaji Wote wa CCM Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, Marafiki pamoja na Ndugu  na  Jamaa wa karibu walioguswa na msiba, na   kuwaomba waendelee kuwa na uvumilivu katika kipindi chote cha msiba huu.
Pia ameiomba  Familia ya Marehemu kuwa na Subra katika kipindi hiki kigumu cha Msiba huu, huku wakiendelea kumuombea dua.
Enzi za uhai wake Marehemu Bw.Maulid Sleyum amefanya kazi katika Afisi Kuu CCM Zanzibar kwa nafasi ya uhudumu.
Marehemu atazikwa kesho kijijini kwao Zingwezingwe Wilaya ya Kaskazini ‘’B”  Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Bw. Maulid Sleyum amezaliwa mwaka 1960 na ameacha kizuka mmoja na watoto watatu.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu pahala Pema Peponi Amin.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.