Habari za Punde

Pasipoti za Kielektoniki zaanza kutolewa Zanzibar

Idara ya Uhamiaji Zanzibar imeanza kutoa pasipoti za kielektroniki kwa wananchi wa Zanzibar wakiwemo viongozi wa serikali kuendeleza zoezi ambalo lilizinduliwa na na Rais wa Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania, Mhe John Pomjbe Magufuli wiki iliyopita.
Pasipoti 11 zilianza kutolewa zikiwemo 6 za kidiplomasia. 
Miongoni mwa waliokabidhiwa Pasipoti zao ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed ambae alikabidhiwa Pasipoti yake na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Katibu Mkuu Kiongozi Dr Abdulhamid Yahya Mzee nae alikabidhiwa pasi yake pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Zubeir Ali Maulid
Wengine waliokabidhiwa pasi zao na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe Omar Othman Makungu, Waziri wa kilimo na Maliasili , Mhe Hamad Rashid Mohammed pamoja na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum, Mhe Juma Ali Khatib.
Mhe Mohammed Abould ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhiwa Pasipoti aliwataka wananchi kutofanya ujanja na kughushi wakati wakiomba hati ya kusafiria na pia aliwataka wahuskia kufanya kazi kwa pamoja ili kulinda nchi yetu.
Waziri Aboud pia aliwakabidhi pasipoti za kielektroniki kwa watendaji wa Serikali Hamida Mussa Khamis na Vuai Iddi Lilla ambae ni Kabu Mkuu wa Shirika la Utalii la Zanzibar.
Pia wananchi wa kawaida waliokabidhiwa Pasipoti zao za kielektroniki na pamoja na Kassim Haidar Jabir pamoja na mwanae anayeitwa Zuleikha, Ali Hamad na Afisa Mawasiliano wa Uhamiaji Bi Tatu Burhan Iddi 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.