Habari za Punde

Serikali Kulipa Madai ya Malimbikizo ya Mishahara Kwa Watumishi wa Umma Kuanzia Kesho.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (hawapo pichani)  kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza na waandishi wa Habari Kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-Bunge mjini Dodoma (Hawapo Pichani)kuhusu hatua ya Serikali ya kuanza kulipa madeni ya malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa Umma, kiasi cha shilingi bilioni 43.39 kuanzia Februari 10, 2018. Kushoto ni Kamishna Msaidizi-Bajeti, Bw. Emmanuel Tutuba na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango (Utawala) Bi. Susan Mkapa, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara hiyo, Bw. Richard Mkumbo (Picha-Wizara ya Fedha na Mipango)

MAELEZO YA MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MALIPO YA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA KWA WATUMISHI
WA UMMA

Ndugu Wawakilishi wa vyombo vya habari, nimewaiteni leo hii ili niwape taarifa fupi kuhusu malipo ya madai ya malimbikizo ya mishahara kwa Watumimishi wa umma waliokuwa na madai ili muweze kuufikishia umma wa Watanzania.

Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management Information System – HCMIS) kufikia tarehe 01 Julai 2017 ilikuwa na madai ya malimbikizo ya mishahara yenye jumla ya shilingi 127,605,128,872.81 kwa watumishi 82,111 Wakiwemo walimu 53,925 waliokuwa wanadai shilingi 53,940,514,677.23  sawa na asilimia 42.27 ya madai yote, na wasiokuwa walimu 28,186 waliokuwa wanadai jumla ya shilingi 73,664,614,195.58 sawa na asilimia 57.73 ya madai yote. Madai haya yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017

Madai haya yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa vyeo na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.

MATOKEO YA UHAKIKI WA MADAI YA SHILINGI BILIONI 127,605,128,872.81 KWA WATUMISHI 82,111

a)  Madai ya watumishi 27,389 kati 82,111 yenye jumla ya shilingi  43,393,976,807.23 ikiwa ni asilimia 34 ya madai yote ya shilingi bilioni 127,605,128,872.81  yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na yanastahili kulipwa bila marekebisho.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.