Habari za Punde

Kamati ya BLW yatembelea kiwanda cha sukari Mahonda

Yataka iruhusiwe kuingia soko la bara
NA ASYA HASSAN
KAMATI ya Bajeti ya Barazala la Wawakilishi, imeitaka wizara ya Biashara na Viwanda, kuhakikisha inalipatia ufumbuzi suala la uingizwaji wa bidhaa zinazozalishwa Zanzibar katika soko la Tanzania bara.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Said Mohamed, alisema hayo baada ya kamati kufanya ziara kutembelea kiwanda cha sukari Mahonda ambapo waliangalia mambo mbalimbali ya kiamendelea na chagamoto.
Alisema ni vyema wizara hiyo kukaa na waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na kulizungumzia suala hilo ili kuona kiwanda cha sukari Mahonda na bidhaa nyengine zinazozalishwa Zanzibar haipati vikwazo vya kuingia katika soko la Tanzania bara.
Aidha alibainisha kuwa upo umuhimu wa kuhakikisha sukari hiyo inapelekwa Tanzania bara kwa sababu ya kupata soko zaidi, kwani Zanzibar haina soko kubwa kutokana na wingi wa watu.
“Tuhakikishe jambo hili tunalipatia ufumbuzi wa haraka kuona bidhaa zetu zinaingiza Tanzania bara, muungano uliopo ni wa nchi mbili ikiwa serikali ya Muungano haitaki tuuingize bidhaa zetu hilo haliwezekani wakati sisi hatukatai vyao kuingia nchini ikiwemo tungule, vitunguu na bidhaa nyengine”, alisema.
Alitaka jitihada zifanyike kuhakikisha kwamba kiwanda sukari Mahonda kinapata soko la Tanzania bara na yapelekwe maombi maalum ili lisijeingizwa suala hilo kwneye kero za muungano.
Hata hivyo alisema, serikali imepitisha sheria ya ZBS, kwa sababu kutaka kuhakikisha biadhaa zinazozalishwa Zanzibar zinakuwa na ubora na viwnago stahiki hivyo upo umuhimu wa biadhaa za Zanzibar nazo kuingia kwneye soko la Tanznaia bara kwa sababu zinakidhi viwango.
Naye Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh, alisema serikali itahakikisha inazitafutia ufumbuzi changamoto zinazokabili kiwanda hicho ikiwemo ardhi, nyumba na ukosefu wa soko Tanzania bara.
“Naamini changamoto hii kwa kushirikiana na wenzetu Tanzania bara inatatuka moja kwa moja, kwani hivi sasa tunataka viwanda na viwanda vinahitaji soko na sisi tuko tayari kuitekeleza sera hiyo na lazima bidhaa tunazozalisha zipate soko ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania bara na hata nje ya Afrika,” alisema.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.