Habari za Punde

Makamu wa Rais Mama Samia aendelea na ziara yake kisiwani Pemba

 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hassan, akipata malezo juu ya ujenzi wa jengo la Mwasisi wa CCM kutoka kwa katibu wa CCM mkoa wa kaskazini Pemba, Khadija Nassor Abdi, wakati alipowasili kajulia hali mwasisi wa CCM Bi Mrashi huko Sizini Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwakabidhi viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, bati kwa ajili ya uwezekaji wa nyumba ya Mwasisi wa CCM Bi Mrashi, huko kijijini kwake Sizini Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) 
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wanaccm na wananchi wa sizini,mara baada ya kujulia hali na kukabidhi bati kwa ajili ya uwezekaji wa nyumba ya mwasisi huo.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 AFISA Mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Shadia Shaaban Seif, akisoma taarifa ya kitaalamu ya ujenzi wa kituo cha huduma ya mama na mtoto huko shumba Vyamboni Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 NAIBU waziri wa Afya Zanzibar Harous Said Suleiman, akizungumzia mikakati ya Wizara yake, mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuweka jiwe la msingi kituo cha huduma za mama na watoto Shumba Vyamboni Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed akizungumza na wananchi wa shumba vyamboni Wilaya ya Micheweni, baada ya uwekwaji wa jiwe la msingi jengo la huduma za mama na watoto.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi wa Shumba Vyamboni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kituo cha huduma za mama na mtoto huko Shumba vyamboni Wilaya ya Micheweni.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akikunjuwa kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi Tawi la CCM Ukunjwi, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mberwa Hamad Mberwa.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


 WANACHAMA waCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakimsikiliza kwa makini makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, wakati alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuweka jiwe la msingi Tawi la CCM Ukunjwi Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)


MAKAMU wa Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza na wananchi na wanaCCM Ukunjwi Wilaya ya Wete, mara baada ya kuweka jiwe la msingi tawi la CCM Ukunjwi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.