Habari za Punde

MBUNGE MARY CHATANDA AKERWA DARASA LA AWALI KUFUNGWA

Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda (kushoto) akiangalia shimo la choo ambalo limeshajengwa na kufukiwa. Ametoa sh. 500,000 kumalizia choo hicho.

Na Yusuph Mussa, Korogwe
IMMAMATUKIO BLOG

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga (CCM) Mary Chatanda ameshangazwa kuona darasa la awali katika Kijiji cha Lwengera- Relini, Kata ya Old Korogwe katika Halmashauri ya Mji Korogwe limekaa miaka saba bila choo.
Matokeo yake, darasa hilo limefungwa na watoto waliokuwa wanasoma hapo imebidi wahamishiwe Shule ya Msingi Lwengera- Darajani na kulazimika kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita sita kila siku kwenda shuleni.

Chatanda ambaye alifika leo Machi mosi, 2018 kukagua shughuli za maendeleo kwenye kijiji hicho, alisema sababu ya Serikali kujenga darasa hilo la awali, ni kuwapunguzia mwenda wa kutembea watoto wa kijiji hicho ambao walikuwa wanalazimika kwenda shule ya msingi kijiji cha jirani cha Lwengera- Darajani.
"Serikali ilikuwa na makusudi kwa kujenga darasa hili, nia ni kuwapunguzia umbali wa kutembea kwenda Lwengera- Darajani, lakini darasa hili miaka saba


Choo hiki cha darasa la awali kijiji cha Lwengera- Relini kina miaka saba ujenzi wake haujakamilika, hivyo kufanya watoto waliokuwa wanasoma hapo kuhamishwa kijiji kingine Lwengera- Darajani. Chatanda ametoa sh. 500,000 ili kukamilisha choo hicho na watoto warudishwe kusoma hapo, ambapo itawapunguzia usumbufu wa kutembea kilomita tatu Shule ya Msingi Lwengera- Darajani, kwenda na kurudi.
Kutokana na darasa la awali katika Shule ya Msingi Lwengera- Relini kufungwa kwa kukosa choo, limeanza kutoa nyufa na kuharibiwa rangi na mchwa. Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda ametoa sh. 500,000 ili kukamilisha choo hicho, huku akiitaka Halmashauri ya Mji Korogwe kukarabati jengo hilo.
Jengo la Darasa la Awali Kijiji cha Lwengera- Relini celling board zake zikiwa zimeachia kutokana na kushindwa kutumika. Ni baada ya watoto waliokuwa wanasoma hapo kuhamishwa kwa kukosa choo.
On Thursday, March 1, 2018, 1:12:41 PM GMT+3, khalfan said wrote:
 NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOSHI
SERIKALI ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuhakikisha wafanyakazi wanalindwa na kupata haki zao pindi wanapopatwa na madhara yatokanayo na kazi, Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde amesema mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro..
 Mheshimiwa Mavunde ameyasema hayo jana (Machi 1, 2018), wakati akiendelea na ziara yake ya kushtukiza ili kuwabaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria linalowataka waajiri wote katika sekta rasmi,(umma na binafsi), waliopo Tanzania Bara kujisajili na kuchangia kwenye Mfuko huo.
Kwa mujibu wa Sheria iliyoanzisha Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, Ikiwa Mwajiri hatajisajili kwenye Mfuko, atakuwa ametenda kosa la jinai kwa mujibu wa kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi na akipatikana na hatia adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000,000 (Milioni Hamsini) au kifungo kisichozidi miaka mitano jela au adhabu zote kwa pamoja, alisema Mhe. Mavunde.
 Mheshimiwa Mavunde ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo Bw. Anslem Peter na Kaimu Kamishna kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, alibaini Mkoa wa Kilimanjaro wenye jumla ya Waajiri 1,039 ni waajiri 525 tu ndio wamejisajili huku wengine 514 bado hawajajisajili na Mfuko.
 “Serikali ilikwishatoa matamko mbalimbali yanayowahimiza waajiri kutekeleza takwa hilo la kisheria, na leo hii hakuna njia nyingine, Waajiri hawa tuliowabaini hapa Mkoani Kilimanjaro naagiza WCF iwapeleke mahakamani haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.” Alisema.
Baadhi ya waajiri ambao Naibu Waziri na timu yake walifanya ukiaguzi huo ni pamoja na kampuni ya Machare Investments, Scholastica Schools iliyoko Himo nje kidogo ya mji wa Moshi.
 Alisema sio lengo la serikali kuwatisha au kuwadhalilisha waajiri hao bali nia ni kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa lakini pia kuwaondolea jukumu waajiri la kuwahudumia wafanyakazi wao wanapopatwa na madhara wakiwa kazini.
 “Tunataka ninyi wawekezaji, (waajiri), mjielekeze kwenye shughuli zenu za msingi kwa maana ya kufanya uwekezaji na biashara zenu na hili la kumuhudumia mfanyakazi aliyepatwa na madhara kazini lishughulikiwe na serikali.” Alisisitiza.
Tayari Mhe. Mavunde amefanya ziara kama hiyo mkoani Mwanza na Shinyanga na kubainisha kuwa operesheni hiyo ya kuwabaini waajiri wasiotekeleza takwa hilo la kisheria litafanyika nchi nzima, na kuwataka waajiri kufanya hivyo haraka ili wasijikute kwenye matatizo.
“Tumewasambaza maafisa wetu wa WCF mikoani na wanaednelea na utaratibu wa kuwafuikisha mahakamani waajiri wote ambao wameshindwa kufuata sheria.
Naibu Waziri ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde(katikati), akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anslem Peter, (kulia) na Mhasibu wa Shule ya Scolastica, Bw.Moshi W.Moshi, wakati wa ziara yake ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi, (WCF) ambapo ilibainika shule hiyo kubwa mjini Moshi haijatekeleza takwa hilo la kisheria
Mhaisbu wa Shule ya Scolastica mjini Moshi, Kilimanjaro Bw. Moshi W. Moshi, na Mkuu wa shule hiyo Bw.Michael Shiloli, wakisikilzia maagizo ya Naibu Waziri Mavunde.
 

 Mkurugenzi  wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika na Afsia Mwandamizi wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bw. Sebere Fulgance.
 Mhe. Mavunde akizungumza na Mkurugenzi wa Machare Investments, (kulia)
 Bw. Anselim Peter akizungujza na waandishi wa habari
 Mhe. Mavunde akisisitiza jambo kwa viongozi wa shule ya Scolastica.
Mkurugenzi  wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, (kulia), akijadili jambo na Kamishna wa kutoka Idara ya Kazi, Bi. Rehema Moyo, (katikati), na   Kaimu Afisa Kazi Mkoa wa Kilimanjaro, Bi.Neema Msyalika 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.