Habari za Punde

Mkutano wa Kikao cha Kampeni ya Maadili

Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (kulia) akifungua kikao cha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) na kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejusha maadili ya mtanzania leo Jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti wa kikundi cha Malezi Daima Bibi. Farida Sabu (Sonia) (kushoto) akichangia mada wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejusha maadili ya mtanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa kikundi cha Malezi Daima Bibi. Hidaya Njaidi (Tusa)
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akizungumza wakati wa kikao na wajumbe wa kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejesha maadili ya mtanzania kwa kuanzia na sekta ya sanaa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha Malezi Daima Bibi. Farida Sabu (Sonia)
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa Bw. Godfrey Mngereza (kulia) akijibu hoja wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejusha maadili ya mtanzania leo Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa kikundi cha Malezi Daima Bibi. Susan Humba (Natasha) (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejusha maadili ya mtanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni mjumbe wa kikundi hicho Bibi. Grace Mapunda (Mama Kawele) 
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akichangia mada wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza na kikundi cha Malezi Daima kujadili namna ya kurejusha maadili ya mtanzania leo Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na wajumbe wa kikundi cha Malezi Daima baada ya kufanya nao kikao cha namna ya kurejesha maadili ya mtanzania hasa katika sekta ya sanaa leo jijini Dar es Salaam. Kulia waliokaa ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo
Picha na: Genofeva Matemu - WHUSM

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.