Habari za Punde

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Yatowa Elimu Kwa Masheha Kisiwani Pemba.

Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Pemba, Ali Salim Ali Matta, akizungumza na masheha wa Wilaya nne za Pemba, juu ya hali halisi ya mwelekeo wa Mvua za masika mwaka huu, kikao kilichofanyika mjini chake chake
Mkurugenzi Mtendaji wa kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar, Shaban Seif Mohamed, akizungumza na masheha wa Wilaya nne za Pemba, juu ya mikakati ya kukabiliana na maafa katika kipindi hiki cha mvua za masika zilizoanza kunyesha katika maeneo mbali mbali ya Pemba
AFISA Operesheni na huduma za binaadamu, kutoka kamisheni ya kukabiliana na maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame akiwasilisha mada juu ya hali ya mwelekeo wa mvua za masika, kwa masheha wa Wilaya nne za Pemba
Mratibu wa Kamisheni ya Kukabiliana na maafa Pemba, Khamis Arazk Khamis akizungumza na masheha wa Micheweni katika kikao cha kukabiliana na maafa kilichofanyika mjini Chake Chake


MASHEHA kutoka Wilaya nne za Kisiwani pemba, wakiwa katika kikao cha siku moja cha kukabiliana na maafa, kilichofanyika mjini Chake Chake, kikiwa na lengo hali halisi ya mwekeo wa mvua za masika mwaka huu.
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.