Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa
Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda
cha Sigara cha Mansoor Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip
Morris Tanzania katika eneo la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga
makofi, wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe
pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha Sigara Mansoor Shanif Hirani.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada
kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiangalia mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa
shughuli mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya
hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda hicho mkoani
Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mojawapo ya
vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya kukifungua.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor
kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii
mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kuhutubia wananchi
waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor
kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii
mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya kutoa
burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi CCM
katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo
Kingolwira mkoani Morogoro
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor
kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu
Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara baada ya kumaliza
kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara cha Mansoor
kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Msanii mkongwe wa
Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akipongezwa na baadhi ya wananchi
mara baada ya kuimba wimbo wake wa Mimi ni Msanii katika sherehe za ufunguzi wa
kiwanda cha Sigara cha Mansoor mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua kiwanda cha
Sigara mkoani Morogoro.
Msanii mkongwe wa
Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika sherehe za
ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia
mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa Mama
Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya
biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.
Mfanyabiashara
mdogo (Machinga) wa Mama Havintoshi
ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya biashara zake
katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na wadau
mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na
Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada kufungua
kiwanda hicho. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment