Habari za Punde

UVCCM wafanya usafi Hospitali ya Chakechake katika kumpongeza Rais Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake

 MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Mkoa Wa wa kusini Pemba, Hanuna Ibrahim Massoud, akishiriki katika upigaji wa deki katika wodi ya watoto iliyomo ndani ya Hospitali ya Chake Chake, wakati wa zoezi la usafi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Chake Chake Pemba, kwa lengo la kumpongeza dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM wakipiga deki katika wodi ya akinamama iliyomo ndani ya Hospitali ya Chake Chake, wakati wa zoezi la usafi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Chake Chake, kwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 VIJANA wa UVCCM Wilaya ya Chake Chake wakifanya usafi kwa kukata majani katika moja ya Wodi ya Hospitali ya Chake Chake, wakati wa zoezi la Usafi lililoandaliwa na Umoja wa  Vijana wa CCM Wilaya hiyo, kwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Chake Chake, wakibeba taka na kwenda kutupa baada ya kumaliza kufanya usafi, katika moja ya wodi za Hospitali ya Wilaya ya Chake Chake, kwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Vijana wa CCM wakifuatia kwa makini hutuba ya ufungaji wa zoezi la usafi wa Hospitali ya Chake Chake, lililoandaliwa na Umoja wa UVCCM Wilaya Chake Chake, kwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
 BAADHI ya Vijana wa CCM wakifuatia kwa makini hutuba ya ufungaji wa zoezi la usafi wa Hospitali ya Chake Chake, lililoandaliwa na Umoja wa UVCCM Wilaya Chake Chake, kwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Mkoa wa kusini Pemba, Hanuna Ibrahim Massoud akimkabidhi madasbin ya kutilia taka, Daktari dhamana wa Haspitali ya Chake Chake Ali Habib, mara baada ya kumalizika kwa zoezi la Usafi likiwa lengo la kumpongeza Dk Shein kutimiza miaka saba ya uongozi wake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.