Habari za Punde

Washindi wa Droo ya tisa ya Promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ wakabidhiwa zawadi zao

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel-Zanzibar, Yussuf Ismali (kushoto) akikabidhi zawadi ya PikiPiki aina ya Boxer kwa mshindi wa droo ya tisa ya Promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ Bw. Rashid Abdallah Hassan, mkazi wa Unguja Zanzibar wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi kuu ya Zantel leo mwishoni mwa juma mjini Zanzibar.
 Afisa Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed Bakar (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Moto C kwa mshindi wa droo ya tisa ya Promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ Bw. Yussuf Masoud Abdulla, mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam na Afisa Mkuu katika Boti za Kilimanjaro za Kampuni ya Azam wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Makao Makuu ya Zantel leo mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Katikati ni Meneja bidhaa wa Zantel, Emilliana Vakolavene.
 Afisa Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed Bakar (kushoto) na mshindi wa zawadi ya simu aina ya Moto C wa droo ya tisa katika Promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ Bw. Yussuf Masoud Abdulla, mkazi wa Temeke jijini Dar es Salaam na Afisa Mkuu katika Boti za Kilimanjaro za Kampuni ya Azam wakiowaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) zawadi hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Makao Makuu ya Zantel leo mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
 Afisa Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed Bakar (katikati) akiwa pamoja na Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Bahati Nasibu nchini, Bakari Maggid akibonyeza kitufe kumpigia moja ya washindi kwenye droo ya tisa ya Promosheni ya JERO YAKO TU iliyofanyika leo mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu. Wengine kwenye picha ni Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Chapa Zantel, Rukia Mtingwa (Kulia) na Afisa Masoko Zantel, Bi. Rehema Cuthbert (Wa pili kulia).
 Afisa Masoko wa Zantel, Hamid Mohamed Bakar (katikati) akisisitiza jambo kwa Mkaguzi Mwandamizi wa Michezo ya Bahati Nasibu nchini, Bakari Maggid (kushoto) na Afisa Masoko Zantel, Rehema Cuthbert (kulia) wakati hafla ya droo ya tisa ya Promosheni ya JERO YAKO TU iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara tu wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.
Meneja wa Mawasiliano na Chapa Zantel, Rukia Mtingwa (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu aina ya Moto C kwa mshindi wa droo ya tisa ya Promosheni ya ‘JERO YAKO TU’ Bi. Zakia Karama Saad, mkazi wa Mkuranga Mkoa wa Pwani wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Makao Makuu ya Zantel leo mwishoni mwa juma jijini Dar es salaam. Promosheni hiyo kabambe ya miezi mitatu imelenga kuwashukuru wateja wa Zantel kwa kuwapa zawadi mbalimbali mara wanapoongeza salio la kiasi cha shilingi 500 tu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.