Habari za Punde

Waziri Mwakyembe akutana na Balozi wa China na Balozi wa Umoja wa Ulaya kuzungumzia masuala ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer wakisalimiana, alipofika ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) pamoja na Bolozi wa Umoja wa Ulaya (katikati) Mhe. Roeland Van de Greer wakiangalia moja ya historia iliyoifadhiwa ya harakati za ukombozi wa Bara la Afrika baada ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimuonyesha Bolozi wa Umoja wa Ulaya (wapili kushoto) Mhe. Roeland Van de Greer pikipiki zilizotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika. Kulia ni Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. WANG KE alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika
 Mratibu wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kushoto) pamoja na wajumbe wengine kutoka Wizara ya Habari wakifuatilia majadiliano ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) na Balozi wa China nchini walipokutana kuzungumzia masuala mbalimbali ya urithi wa ukombozi wa bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia kitabu alichopewa na balozi wa China nchini Mhe. WANG KE (kushoto) baada ya kufanya mazungumzo yanayohusu masuala ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.