Habari za Punde

Mafunzo ya Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na kutumia Vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi kuchochea Uwajibikaji wa Watendaji

AFISA Miradi wa TAMWA Zanzibar Bi. Asha Abdi akifungua mafunzo ya Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na kutumia Vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi kuchochea Uwajibikaji wa Watendaji, yaliowashirikisha Waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar na watumiaji wa Mitandao ya Kijamii Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Watu wenye Ulemavu Welesi Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar Jabir Idrisa akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliuofanyika katika ukumbi wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar,Welesi.
BAADHI ya Waandishi wa wakifuatilia Warsha ya Siku moja ya Mafunzo ya kuwawezesha Waandishi wa habari kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi na kuchochea uwajibikaji wa Watendaji, yaliofanyika katika ukumbi wa Watu wenye Ulemavu welesi, yalioandaliwa na Tamwa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar
MTOA Mada kutoka Chuo Kikuu cha SUZA Mwalimu Seif Gharib akitowa mata ya kuhusiana na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii kuhabarisha Wananchi, wakati wa warsha ya mafunzo ya Siku moja kwa Waandishi wa Habari Zanzibar yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar,(WAHAMAZA) yaliofanyika katika ukumbi wa watu wenye ulemavu welesi Zanzibar
MTOA Mada Mwalimu Burhani Muhuzi,akitowa mada kuhusiana na Nguvu ya Mitandao ya Kijamii, wakati wa warsha ya siku moja ya mafunzo kwa Waandishi wa habari kuhusiana na kuwawezesha waandishi kutumia mitandao ya kijamii kupazac sauti za wananchi na kuchochea uwajibikaji wa Watendaji, warsha hiyo imeandaliwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na WAHAMAZA,iliofanyika katika ukumbi wa watu wenye ulemavu welesi Zanzibar

NAIBU Mkurugenzi wa Idara ya Habari Zanzibar. Dkt. Juma Mohammed Salum, akifunga mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusiana na matumizi ya mitandao ya kijamii, mafunzo yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar kwa Jumuiya ya Wandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA)yaliofanyika katika ukumbi wa Watu wenye ulemavu welesi Zanzibar
BAADHI ya Waandishi wa wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Mohammed Salum akifunga mafunzo hayo ya Siku moja kuwawezesha Waandishi wa habari kutumia vyombo vya habari pamoja na mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi na kuchochea uwajibikaji wa Watendaji, yaliofanyika katika ukumbi wa Watu wenye Ulemavu welesi, yalioandaliwa na Tamwa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar Salma Said akizungumza wakati wa ufungaji wa Warsha hiyo ya Siku Moja iliowashirikisha Waandishi wa Habari Zanzibar, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Watu Wenye Ulemavu Zanzibar,Welesi.
Waandishgi wa Habari walioshiriki Mafunzo ya Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na kutumia Vyombo vya habari pamoja na Mitandao ya Kijamii kupaza sauti za Wananchi kuchochea Uwajibikaji wa Watendaji, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mafunzo hayo yaliofanyika katika Ukumbi wa Watu wenye Ulemavu Welesi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.